VIEW OTHER SITES

Thursday

AHMED HASSAN NA MISRI KUJIFUNGIA NA MSUMBIJI


Cafonline.com: Unautazamaje mchezo wa Ijumaa(Leo) dhidi ya         Msumbiji?
 
Hassan: Utakuwa mgumu. Kwanza mara nyingi wamekuwa wagumu hasa mechi za kufuzu. Na hali ya sasa inaufanya kuwa mgumu zaidi maana tunacheza milango ikiwa imefungwa na tunakosa soka la haswa kutokana na hali ya amani Misri. Ila tunatazamia kupata ushindi.
 
Cafonline.com: Unalizungumziaje kundi lenu mkiwa na Msumbiji, Guinea na Zimbabwe?

Hassan: Tunaziheshimu timu zote bila kuangalia majina yao. Soka la Afrika limekuwa sana kwa ubora bila kujali nchi. Mwaka huu tulipoteza dhidi ya Niger, Sierra Leone mbali na kuwa chini sana kwa ubora ukilinganisha na sisi wakati huo.
 
Cafonline.com: Unadhani mtaathirika kucheza bila mashabiki wenu?

Hassan: Tunatumaini mambo yatabadilika Misri na tutakuwa na mashabiki wetu. Lakini kwa sasa tunakubali kucheza bila mashabiki kutokana na hali ya usalama. Naamini hatutaathirika kwa kiwango kikubwa kutokana na kuwakosa mashabiki wetu.
 
Cafonline.com: Ukiwa kama nahodha una ujumbe gani kwa wachezaji wenzio?
 
Hassan: Wachezaji wote wanajua wajibu wao na wanafikiria zaidi mchezo huu. Tuna imani tutapata ushindi ili kuwafurahisha wamisri wote.

Mechi nyingine hii leo ni GHANA v LESOHO itayochezwa mji wa Kumasi.











STARS,IVORY COAST KUPIGWA SAA 2 USIKU ZA AFRIKA MASHARIKI



Zikiwa zimebaki saa nne kabla kikosi cha timu ya taifa ya wanaume(soka) Taifa Stars kukwea pipa kuelekea Ivory Coast kwa mchezo wa kimataifa wa kufuzu fainali za kombe la dunia 2014 nchini Brazil timu hiyo itawakosa nyota wawili.

Stars yenye kikosi cha wachezaji 23 na viongozi 9 inatarajia kuondoka saa 11.10 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kwenda Abidjan kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia itakayochezwa Juni 2 mwaka huu.

Wachezaji walio kwenye orodha hiyo ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Nassor Masoud Cholo, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe na Juma Nyoso.

Wengine ni Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva, Haruna Moshi na John Bocco.

Wanaobaki kwa kuwa na majeruhi ni mshambuliaji Thomas Ulimwengu anayechezea klabu ya TP Englebert Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari.

Viongozi wanaoondoka na timu ni Kocha Mkuu Kim Poulsen, Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Mukebezi (Meneja wa timu), Juma Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Daktari wa mifupa) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

Msafara unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Crescentius Magori huku msaidizi wake akiwa Makamu wa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) Haji Ameir Haji.

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala akiwaaga wachezaji hao aliwataka kwenda kuiwakilisha vyema Tanzania kwenye mchezo huo wakati wa hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi, Rais wa TFF, Leodegar Chilla Tenga na Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe ambao pia ni wadhamini wa Taifa Stars.

Mechi hiyo itachezwa saa 11 kamili kwa saa za Ivory Coast sawa na saa 2 kamili usiku Afrika Mashariki kwenye uwanja wa kumbukumbu wa Felix Houphouet-Boigny aliyekuwa rais wa kwanza wa Ivory Coast ukichukua mashabiki 40,000.

Mwamuzi wa kati ni Slim Jedidi,mwamuzi msaidizi namba moja ni Bechir Hassani, wote kutoka Tunisia,mwamuzi msaidizi namba mbili ni Sherif Hassan kutoka Misri na mwamuzi wa akiba ni Youssef Essrayri pia kutoka Tunisia.

Mtathmini wa waamuzi ni Rachid Medjiba kutoka Algeria wakati Kamishna wa pambano hilo atakuwa Saleh Issa Mahamat kutoka Chad.

Stars itarajea nchini Juni 5 mwaka huu saa 1.40 asubuhi na kuingia kambini kwa maandalizi ya mechi dhidi ya Gambia itakayochezwa Juni 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


PASI ZA SWANSEA ZAMSHUSHA BRENDAN ANFILED


Brendan Rodgers


RODGERS BRENDAN
Tarehe ya kuzaliwa:
(1973-01-26) 26 January 1973 (age 39)
Mahali pa kuzaliwa:
Nafasi aliyoichezea:
Mlinzi
Taarifa za Klabu
Klabu ya sasa:
Liverpool (KOCHA)
Timu ya utotoni
1984–1987
Timu ya wakubwa
Mwaka
Timu
Mechi
Magoli
1987–1990
12
(1)
1990
0
(0)
Timu alizofundisha
2008–2009
2009
2010–2012
2012–

Tuesday

REKODI KUELEKEA EURO 2012


MCHEZAJI MKUBWA ZAIDI
KOSTAS CHALKIAS – 30 MEI 1974 (38)
GOLIKIPA
ANACHEZEA TIMU YA TAIFA YA UGIRIKI NA
KLABU YA PAOK SALONIKA YA UGIRIKI.

MCHEZAJI MDOGO ZAIDI
 JETRO WILLEMS – 30 MACHI 1994 (18)
BEKI
ANACHEZEA TIMU YA TAIFA YA UHOLANZI NA
KLABU YA PSV EINDHOVEN YA UHOLANZI.

MCHEZAJI ALIYECHEZA MECHI NYINGI KIMATAIFA
IKER CASILLAS – 20 MEI 1981
GOLIKIPA
ANACHEZEA TIMU YA UHISPANIA NA AMECHEZA MECHI
129.
WACHEZAJI WANAOCHEZA NJE YA ULAYA
 1. CHRISTIAN WILHELMSSON
ANACHEZEA KLABU YA AL HILAL YA SAUDI ARABIA NA
TIMU YA TAIFA YA SWEDEN.
 2. ROBBIE KEANE
ANACHEZEA KLABU YA LOS ANGELES GALAXY YA MAREKANI NA
TIMU YA TAIFA YA IRELAND KASKAZINI.




Monday

UPANGAJI MATOKEO CONTE MATATANI ITALIA

Kocha wa klabu ya Juventus mabingwa wa Serie A ameingia matatani kwa tuhuma za kuhusika na upangaji wa matokeo nchini humo.
Tukio hilo limepelekea kukamatwa kwa nahodha wa klabu ya Lazio, Stefano Mauri mwenye miaka 32 kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tukio hilo akiwa pamoja na nahodha mstaafu na kiungo wa Genoa, Omar Milanetto.
Maafisa wa polisi walienda kwenye kambi ya timu yataifa ya Italia ili kufanya mahojiano na beki wa kushoto wa Italia na klabu ya Zenit St. Petersburg ya Urusi, Domenico Criscito mwenye miaka 25.
Hata polisi nchini humo bado inatafuta makazi 30 ya wachezaji, wakufunzi na viongozi wa vilabu vinavyoshiriki ligi za nchini huma ikiwemo Serie A, Serie B na madaraja ya chini.
Polisi imesema Conte anashikiliwa kutokana na kuhusishwa na upangaji matokeo akiwa na klabu yake ya zamani Siena wakati ikicheza na Novara Aprili,2011, hata hivyo wakili wa Conte, Antonio De Rencis, amesisitiza kuwa mteja wake hausiki na tukio lolote la upangaji matokeo nchini humo.
Naye makamu wa rais wa shirikisho la soka nchini humo, Demetrio Albertini ametangaza kuwa Cristico ambaye ni beki wa zamani wa Genoa na Juventus hatochaguliwa kwenye kikosi kitakachoshiriki michuano ya Ulaya nchini Ukraine na Poland hadi atakapoonekana hana hatia.
Wengine waliokumbwa na mkasa huo ni Leonard Bonucci beki wa Juventus alipokuwa na klabu ya Bari.

NOMVETHE ATAWALA TUZO ZA ABSA

Mshambuliaji wa Moroka Swallows, Siyabonga Nomvethe amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa 2011/2012 kwenye ligi kuu Afrika ya Kusini zilizofanyika kwenye ukumbi wa Gold Reef City hapo jana.
Nomvethe mwenye miaka 34 pia alishawahi kutwaa tuzo hizo msimu wa 1999/2000 alipotwaa tuzo mbili za ligi kuu nchini Afrika Kusini.
Mbali na tuzo hizo Nomvethe amefanikiwa kutia kibindoni
jumla ya shilingi.

Absa mchezaji bora wa mwaka – R150 000
Siyabonga Nomvethe
*Absa mchezaji wa wachezaji wa msimu– R150 000
Siyabonga Nomvethe
*Absa mlinda mlango bora wa msimu – R50 000
Wayne Sandilands
*Absa Premiership Red Hot mchezaji chipukizi – R50 000
Ronwen Williams
*Absa Premiership kocha bora wa msimu – R75 000
Gordon Igesund
*Absa Premiership Absa-goli bora la msimu – R50 000
*Benni McCarthy
Absa Mfungaji bora –  R50 000
*Siyabonga Nomvethe
Nedbank- Mfungaji bora – R50 000
*David Radebe
Nedbank – Mchezaji wa Mashindano – R100 000
*Nyasha Mushekwi
Nedbank-Mchezaji chipukizi wa mashindano – R25 000
*Thabiso Nkoana
Telkom – Mchezaji bora wa mashindano – R200 000
*Benni McCarthy
MTN8 Mchezaji bora – R150 000
*Oupa Manyisa
Mwamuzi wa bora – R50 000
*Victor Hlungwani
Mwamuzi bora msaidizi – R40 000
*Zakhele Siwela - Winner

ZESCO YAENDELEA KUONGOZA LIGI KUU ZAMBIA


Klabu ya Zesco United imefanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini Zambia baada ya kuifunga National Assembly kwenye uwanja wa Mwanawasa kwa 1-0 wakifikisha alama 27 kwa ushindi huo.
Zesco walipata ushindi wao kupitia kwa Kondwani Mtonga ikiunganisha krosi ya Innocent Mwiba dakika ya 75 akiwazidi ujanja mabeki wa National Assembly kuifanya tiu hiyo kuweka wigo wa alama nne mbele ya Zanaco yenye alama 23.
Hata hivyo Zesco walikosa nafasi ya wazi dakika ya 6 wakati Alfred Luputa akipiga krosi ambayo ilimshinda mlinda mlango wa National Assembly, Phillip Banda lakini washambuliaji wa Zesco wakikosa umakini kumalizia krosi hiyo.
Mchezo huo pia ulishuhudiwa kwa kocha wa Zesco, Wedson Nyirenda alipewa kadi nyekundu baada ya kumtolea mwamuzi, Joseph Jere maneno machafu kufuatia mchezo mbaya aliofanyiwa Jackson Mwanza.

WEBBER ATWAA UBINGWA MONACO GP

Dereva wa Red Bull, Mark Webber amefanikiwa kutwaa taji la mbio za magari za Monaco nchini Ufaransa kwa mara ya pili kwa kuwazidi Fernando Alonso wa Ferrari na Nico Rosberg wa Mercedes Benz.
Mbio hizo zenye umbali wa kilomita 3.340 sawa na maili 2.075 zilishuhudiwa kwa muaustralia, Webber akitwaa ubingwa wake wa pili wa Monaco GP akitumia muda wa 1:18.805.
WALIOINGIA KWENYE TANO BORA NA MUDA WALIOTUMIA
DEREVA                    TIMU             MUDA
1    Mark Webber         RED BULL         1:18.805
2    Nico Rosberg        MERCEDES BENZ    1:18.977
3    Fernando Alonso    FERRARI          1:18.857
4    Sebastian Vettel   RED BULL         1:19.076
5    Lewis Hamilton      McLAREN          1:18.806
Mbali na ushindi huo wa Webber katika viunga vya Monte Carlo na kutwaa taji kutoka kwa Vettel bingwa wa 2011 bado rekodi ilitowekwa na Michael Schumacher mwaka 2004 akitumia muda wa 1:14.439 ilishindwa kuvunjwa na Webber akizidiwa kwa sekunde 4.366.
Mwaka jana katika mbio za Monaco Webber alishika nafasi ya nne akitumia 1:16.234 nyuma ya Button, Alonso na Vettel.
Kwa ushindi huo Webber amejitwalia alama 25.

KAMATI YA UCHAGUZI TFF YATOA AGIZO KWA YANGA

Kikao cha kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake, Deogratias Lyatto kimejadili mustakabali wa nafasi za uongozi ndani ya klabu ya Yanga kufuatia kujiuzuru kwa wajumbe nane na mmoja kufariki dunia kati ya wajumbe 13, hivyo kutoa ufafanuzi na kuipa maagizo Kamati ya Uchaguzi ya Yanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipokea ushauri wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF na kutoa ufafanuzi na maagizo yake ikiwemo kuitaka Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuanza mchakato wa kujaza nafasi za wazi za Kamati ya Utendaji kwa mujibu wa Katiba ya Yanga Ibara ya 28.
Mchakato huo umetakiwa kuanza mapema  Juni mosi na Julai 15 uchaguzi ufanyike kuziba nafasi zilizoachwa na wajumbe walijuizuru baada ya kupangwa mahali pa kufanyia uchaguzi huo na Kamati ya Uchaguzi wa Yanga kwa kushirikiana na Sekretariati ya Yanga.
Vile vile Kamati ya Uchaguzi ya TFF imesisitiza kuwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi uwe na ajenda moja tu ya Uchaguzi ili kujaza nafasi za wazi za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga.
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliobaki kwenye nafasi zao hadi sasa ni Sarah Ramadhan, Mohamed Bhinda, Tito Osoro na Salim Rupia.

MATOKEO TENISI – ROLAND GARROS, UFARANSA


RAUNDI YA KWANZA:
Lukasz Kubot (POL) v Karol Beck (SVK)
 7-5, 6-2, 4-4
x31-Kevin Anderson (RSA) v Rui Machado (POR),
 7-6(2), 6-7(6), 4-6, 6-1, 7-7
Nicolas Devilder (FRA) v Filip Krajinovic (SRB)
6-2, 6-2, 6-0
Michael Berrer (GER) v x30-Jurgen Melzer (AUT)
 6-7(5), 4-6, 6-2, 6-2, 6-3
Gilles Muller (LUX) v Igor Sijsling (NED)
 2-6, 7-5, 3-6, 6-4, 8-6
Nicolas Mahut (FRA) v x26-Andy Roddick (USA)
6-3, 6-3, 4-6, 6-2
x5-Jo-Wilfried Tsonga (FRA) v Andrey Kuznetsov (RUS)
 1-6, 6-3, 6-2, 6-4
Pablo Andujar (ESP)v Victor Hanescu(ROU)
 6-1, 2-6, 1-6, 6-3, 6-1
x14-Fernando Verdasco (ESP)vSteve Darcis(BEL)
 6-3, 6-2. 7-6(4)
x18-Stanislas Wawrinka (SUI) v Flavio Cipolla (ITA)
 6-3, 6-3, 4-6, 3-6, 6-2
Edouard Roger-Vasselin (FRA) v Vasek Pospisil (CAN)
 3-6, 6-3, 6-2, 6-2
x9-Juan Martin Del Potro (ARG) v Albert Montanes (ESP)
 6-2, 6-7(5), 6-2, 6-1
Juan Carlos Ferrero(ESP)v Jonathan Dasnieres De Veigy (FRA) 6-1, 6-4, 6-3
Cedrik-Marcel Stebe (GER) bt Joao Souza (BRA)
 6-3, 2-0 Ret.
x21-Marin Cilic (CRO) bt Daniel Munoz-De La Nava (ESP)
 6-4, 6-4, 7-5
Fabio Fognini (ITA) bt Adrian Mannarino (FRA)
 6-0, 7-5, 6-1

MECHI KALI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014 WIKI HII


IJUMAA – 01/06/2012
Ghana     V     Lesotho     
Egypt     V     Mozambique  
JUMAMOSI
Kenya     V     Malawi
Cameroon V     Congo DR      
Tunisia V  Equatorial Guinea         
Sudan     V     Zambia      
Côte d'Ivoire V     Tanzania         
Algeria   V     Rwanda      
JUMAPILI – 03/06/2012
South Africa V     Ethiopia         
Angola    V     Uganda      
Togo      V     Libya       
Nigeria   V     Namibia     

GEBRSELASSIE ASHINDWA KUFUZU OLIMPIKI 2012

Bingwa wa zamani wa mita 10,000 duniani raia wa Ethiopia, Haile Gebrselassie ameshindwa kufuzu kwa mashindano ya Olimpiki ya London, Uingereza baada ya kushika nafasi ya saba kwenye mashindano ya Fanny Blankers-Koen yaliyofanyika Hengelo, Uholanzi.
Gebrselassia mwenye miaka 39 alimaliza mbio hizo kwa dakika 27 na sekunde 20.39 huku mshindi Tariku Bekele kutoka Ethiopia akitumia dakika 27 sekunde 11.70 katika mashindano hayo yaliyoandaliwa maalumu ili kupata wawakilishi wa Ethiopia kwenye mashindano ya Olimpiki.
Wanariadha wengine waliungana na Bekele ni Leleisa DEsisa Benti aliyeshika nafasi ya pili, huku nafasi ya tatu ikienda kwa Kenenisa Bekele.
Gebrselassie  mshindi wa mbio za Great Manchester wiki iliyopita ameshindwa kufuzu kwa mashindano yake ya tano ya Olimpiki huku akifanikiwa kushinda medali za dhahabu mwaka 1996 na 2000 mbio za mita 10,000.
Matokeo mengine,
Wanaume

100m (0.5 m/s)
 1. Churandy Martina (NED) 10.18
 2. Mario Forsythe (JAM) 10.25
 3. Ainsley Waugh (JAM) 10.31
400m:
 1. Luguelin Santos (DOM) 44.45
 2. Martyn Rooney (GBR) 44.97
 3. Nery Brenes (CRC) 45.20
5. Oscar Pistorius (RSA) 46.35
800m:
 1. Adam Kszczot (POL) 1:43.83
 2. Timothy Kitum (KEN) 1:44.00
 3. Job Kinyor (KEN) 1:44.17
1500m:
 1. Nixon Chepseba (KEN) 3:29.90
 2. Ayanleh Souleiman (DJI) 3:30.31
 3. Mekonnen Gebremedhin (ETH) 3:31.45
10000m:
 1. Tariku Bekele (ETH) 27:11.70
 2. Leleisa Benti (ETH) 27:11.98
 3. Sileshi Sihine (ETH) 27:12.60
 7. Haile Gebrselassie (ETH) 27:20.39
110m hurdles:
 1. Ronnie Ash (USA) 13.31
 2. Andrew Pozzi (GBR) 13.39
 3. Arthur Noga (POL) 13.45
Wanawake
200m:
 1. Charonda Williams (USA) 22.73
 2. Jamile Samuel (NED) 22.93
 3. Tiffany Towsend (USA) 23.04
800m:
 1. Janeth Jepkosgei (KEN) 1:57.79
 2. Yuneysi Santiusti (CUB) 1:58.53
 3. Annet Negesa (UGA) 1:59.08
1500m:
 1. Hanna England (GBR) 4:04.05
 2. Corina Harrer (GER) 4:04.81
 3. Laura Weightmann (GBR) 4:04.88
100m hurdles:
 1. Kellie Wells (USA) 12.81
 2. Lolo Jones (USA) 12.90
 3. Queen Harrison (USA) 12.98
Discus
 1. Zaneta Glanc (POL) 64.71m
 2. Sendriute Zinaida (LIT) 62.74
 3. Joanna Wisnewska (POL) 59.50

KOTOKO YATWAA UBINGWA GHANA

Klabu kongwe nchini Ghana ya Asante Kotoko imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2011/2012 nchini humo hii leo.
Timu hiyo imetwaa ubingwa huo baada ya kuifunga Tema Youth kwa goli moja bila majibu kupitia kwa Richard Yeboah iliyeunganisha krosi ya Kofi Nti_Boakye kutokea wingi ya kushoto dakika ya 57.
Mchezo huo uliopigwa kwenye mji wa Kumasi ulishudiwa na mashabiki lukuki wa Kotoko ambapo beki wa kushoto wa Kotoko, Gideon Baah alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo kutokana na kiwango alichokionesha kwa kuisumbua timu ya Tema Youth.
Kocha wa KOtoko, Maxwell Konadu alimjumuisha Ben Acheampong kwenye kikosi chake hii leo ambaye ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ghana “Black Stars” kitakachoikabili Lesotho mwishoni mwa wiki hii.
Nafasi ya pili imeenda kwa Ashanti Gold iliyofikisha alama 47 baada ya kuifunga Ebusua Dwarfs magoli 2-0 kwenye uwanja wa Sekondi kupitia kwa Mohamed Yakubu.
Matokeo mengine na miji ilikochezwa michezo hiyo,
Accra: Hearts 4-0 Arsenals
Dormaa: Aduana 1-0 Liberty
Wa: A. Stars 1-0 Medeama
Bekwai: New Edubiase 1-0 Bechem Utd
Berekum: Chelsea 1-1 Mighty Jets


MSIMAMO MZIMA BAADA YA KUMALIZA KWA LIGI HIYO HII LEO;
1    Asante Kotoko 30   18   9    3    42   18   24   59
2    AshantiGold FC 30   13   10   7    34   33   1    48
3    Adunana Stars 31   11   14   6    25   15   10   47
4    Hearts of Oak 30   13   10   7    31   19   12   46
5    Medeama SC    30   13   5    12   39   34   5    44
6    Liberty Professionals   30   11   9    10   38   29   9  42
7    Berekum Chelsea    30   11   12   7    30   23   7    41
8    Edubiase FC   30   13   5    12   34   36   -2   38
9    Tema Youth    30   9    9    12   31   30   1    35
10   WA All Stars  30   10   10   10   19   20   -1   34
11   Dwarfs    30   9    10   11   23   25   -2   33
12   Arsenals  31   7    10   14   24   40   -16  31
13   Heart of Lions 30   7    11   12   21   31   -10  29
14   Wassaman United    30   7    8    15   27   42   -15  29
15   Mighty Jets   30   5    14   11   23   29   -6   28
16   Bechem United 30   5    12   13   24   41   -17  27

FIFA yatoa onyo kwa KFF

Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetoa tahadhari kwa shirikisho la soka nchini Kenya kusimamia usalama wa mchezo wake na Malawi utakaofanyika wikendi hii uwanja wa Nyayo.
Mchezo huo ni wa mchujo ili kupata nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014 ambapo Kenya itacheza na Malawi Juni 2 mwaka huu.
FIFA imetoa tahadhari hiyo kufuatia vitendo vya ulipuaji mabomu vinavyofanyika kwenye nchi huku kundi la kigaidi kutoka nchini Somalia, Al-Shabaab likihusishwa na mashambulio hayo.
Mwaka jana FIFA waliufungia uwanja wa Nyayo kutokana na kuingiza watu zaidi ya idadi inayotakiwa vurugu baina ya mashabiki, hivyo kulitaka shirikisho kusimamia utulivu na usalama ili kuepuka kufungiwa kufanyika kwa mchezo wowote wa kimataifa nchini humo.


Saturday

NYOTA ATLETICO ANAYENG'ARISHA MCHEZO WA STARS DHIDI YA THE FLAMES


JINA: ROBIN NGALANDE
TAREHE YA KUZALIWA: NOVEMBA, 2, 1992.
TAIFA: MALAWI.
KLABU: ATLETICO DE MADRID, UHISPANIA (MKOPO)
NAFASI: MSHAMBULIAJI.
UREFU: 1.70 M (5ft7 in)
MWAKA           TIMU
2009            CIVO UNITED, MALAWI
2009 -2010      MAMELODI SUNDOWNS, AFRIKA KUSINI.
2010 -          ATLETICO DE MADRID, UHISPANIA.
TIMU YA TAIFA
MWAKA     TIMU     MECHI    MAGOLI
2010 -    MALAWI     1       0

Ngalande yupo chini ya Sport Agency kampuni ambayo pia ni wakala wa Benni McCarthy, amecheza mechi moja ya kimataifa na timu ya Malawi “The Flames” mnamo Julai,6, 2010 kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa nchi hiyo dhidi ya Lesotho iliyopigwa uwanja wa Civo uliopo mji mkuu wa nchi hiyo, Lilongwe.
Mwaka 2010 alishiriki michuano ya vijana U-18 nchini Uhispania akiwa na kikosi cha vijana cha Sondowns huku akifunga magoli mawili kwenye mechi tatu, kabla ya kutolewa hatua ya robo fainali na Boca Junior ya Argentina.
Miongoni mwa vilabu vilivyowahi kumtaka kinda huyo wa Malawi ni pamoja na Chelsea, Manchester City na Espanyol.