Timu ya taifa ya
Misri hapo jana ilifanikiwa kupata ushindi wa 2 -0 dhidi ya Msumbiji kwenye
mchezo wa kufuzu ili kushiriki kombe la dunia 2014 nchini Brazil kwenye uwanja
wa jeshi jijini Alexandria.
Ushindi kama huo
iliupata mwaka 1990 dhidi ya Msumbiji, huku mlinzi Mahmoud Fathallah alifunga
goli la kwanza kabla ya mlinda mlango Joao Kampango akijifunga mwenyewe na
kuwapa Misri uongozi wa kundi G lenye timu zingine za Zimbabwe na Guinea
zitakazocheza hapo kesho jijini Harare, Zimbabwe.
Misri mabingwa wa
mara 7 barani Afrika wameshiriki fainali za kombe la dunia mara 2.
Nayo nchi ya Ghana
chini ya kocha mzawa Kwesi Appiah ilipata ushindi mnono wa magoli 7-1 kwenye
kundi D lenye miamba ya Afrika 2012, Zambia na Sudan, Ghana ilipata magoli yake
kupitia kwa Sulley Muntari, Christian Atsu, Jeremiah Akaminko (1),huku Dominic Adiyah na Jordan Ayew (2) kila mmoja.
Hii leo kutakuwa
michezo kadhaa ikiwa na saa za hapa Tanzania kuanzia saa 10 kati ya Kenya dhidi
ya Malawi hadi nne usiku Rwanda wakiikabili Algeria.
| 10:00 | Kenya | v | Malawi | Nairobi |
| 11:00 | Central African Republic |
v | Botswana | Bangui |
| 11:30 | Cameroon | v | Congo DR | Yaounde |
| 01:30 | Sierra Leone | v | Cape Verde | Freetown |
| 01:30 | Gambia | v | Morocco | Bakau |
| 02:00 | Sudan | v | Zambia | Khartoum |
| 02:00 | Ivory Coast | v | Tanzania | Abidjan |
| 02:00 | Tunisia | v | Equatorial Guinea | Monastir |
| 03:00 | Burkina Faso | v | Congo | Ouagadougou |
| 03:00 | Senegal | v | Liberia | Dakar |
| 04:30 | Algeria | v | Rwanda | Blida |