VIEW OTHER SITES

Sunday

CZECH, UGIRIKI ZAWASILI POLAND

Timu za taifa za Czech na Ugiriki zimekuwa za kwanza kufika nchini Poland kwa michuano ya Ulaya 2012 huku ikiwa zimebakia siku tano kabla ya kunza kwa michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.
Timu zote zimepangwa kundi moja la A pamoja na Poland na Urusi, ambapo mechi za kwanza zinatarajiwa kuchezwa ijumaa wiki hii kwa Poland kufungua dimba na bingwa wa 2004,Ugiriki kwenye mji mkuu Warsaw huku Urusi akicheza na Jamhuri ya Czech kusini magharibi mwa mji wa Wroclaw.
Jamhuri ya Czech imewasili Wroclaw kutokea Prague kwa usafiri wa garimoshi lenye rangi nyekundu, nyeupe na bluu zinazovaliwa na timu hiyo zikiwemo kwenye bendera ya taifa lao, huku Ugiriki wakiwasili kwenye mji wa Warsaw.
Czech wataingia uwanja wakiwa na nahodha wao, Thomas Roscicky aliyepata majeraha madogo ambapo madaktari wa timu wamethibitisha kuwa atashiriki kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Urusi huku akitarajiwa kukutana na nahodha wa Urusi na mchezaji mwenzake wa zamani wa   Arsenal, Andrey Arshavin.
Hata hali ya usalama inaelekea kutiwa doa nchini humo kufuatia mpango wa kufanya maandamano ulioandaliwa na kikundi cha watu wanaoipinga serikali mpya ya Bronislaw Komorowski waliopanga kuandamana Juni, 10.


MGOSI KUSAJILI JANGWANI


Mshambuliaji wa Daring Club Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mussa Hassan Mgosi ametua nchini akitokea nchini Congo DR kutokana na kuendelea kwa mechi za kimataifa za kufuzu kucheza kombe la dunia 2014 zinazoendelea kwenye nchi mbalimbali barani Afrika.
Hata hivyo Mgosi anahusishwa na mipango ya kujiunga klabu ya Yanga ambayo ipo kwenye mchakato wa kupata viongozi wapya wa klabu hiyo kwa sasa.
Kwa upande wake Mgosi ambaye amepata kuzitumikia timu mbalimbali nchini zikiwemo Simba SC, Moro United akitokea shule ya sekondari ya Makongo amekana taarifa hizo kwa maelezo kuwa amekuja kutokana na matatizo ya kifamilia na atarejea DRC baada ya wiki mbili.

STARS YAANZA KUJIFUA IKIWA IVORY COAST


Timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeanza kujifua ikiwa Ivory Coast kujiandaa na mechi ijayo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia 2014 nchini Brazil, dhidi ya Gambia itakayochezwa Jumapili ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kocha Mdenmark, Kim Poulsen, leo aliiongoza Taifa Stars kufanya mazoezi asubuhi kwenye uwanja wa Shirikisho la Soka la Ivory Coast (FIF) pembezoni mwa jiji la Abidjan.
Timu hiyo itafanya tena mazoezi kesho (Juni 4 mwaka huu) asubuhi kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani saa 1.30 usiku kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi ambapo itawasili Dar es Salaam, Juni 5 mwaka huu saa 1.40 asubuhi.
Kocha Kim aliwakosa wacheaji wanne ambao ni majeruhi (Thomas Ulimwengu, Nurdin Bakari, Haruna Moshi na Nassoro Masoud Cholo) amesema hivi sasa wameelekeza mawazo yao kwenye mechi ijayo dhidi ya Gambia.
“Safari ya kujenga timu ndiyo imeanza. Mechi dhidi ya Ivory Coast imepita na ninawashukuru wachezaji kwa kucheza kwa mujibu wa maelekezo na kujituma. Mpira ni mchezo wa makosa, tumefanya makosa yaliyosababisha tuwape Ivory Coast mabao mepesi.
“Lakini kama nilivyosema mechi hiyo imepita, hivi sasa tunaangalia mechi ijayo dhidi ya Gambia. Hatuna muda mwingine wa kujipanga na ndio maana niliamua kuja na wachezaji wote Abidjan,” amesema Kim.
Mechi dhidi ya Gambia itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni. Gambia ilitoka sare ya bao 1-1 na Morocco katika mechi iliyochezwa juzi jijini Banjul.
Taifa Stars itamkosa na nahodha msaidizi, Aggrey Morris aliyeoneshwa kadi nyekundu dakika ya 65 baada ya kupata ya pili ya njano kwenye mechi dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan.

MCHEZAJI WA KWANZA MWEUSI KUCHEZA JAMHURI YA CZECH



Theodor Gebre Selassie
TAARIFA BINAFSI
Full name
Theodor Gebre Selassie
Date of birth
24 December 1986 (age 25)
Place of birth
Height
1.82 m (6 ft 0 in)
Playing position
TAARIFA ZA KLABU
KLABU YA SASA
NAMBA
32
TIMU ZA UTOTONI
1992-1998
FC Velké Meziříčí
1998-2005
TIMU ZA UKUBWANI
MWAKA
TIMU
MECHI
(GOLI)
2005–2007
18
(2)
2005–2006
→ FC Velké Meziříčí (Loan)
8
(0)
2007–2008
11
(0)
2008–present
80
(5)
TIMU YA TAIFA
2007–2008
6
(0)
2011–
8
(0)
*
THEODOR NDO MCHEZAJI WA KWANZA KUITUMIKIA NCHI YA CZECH AKIZALIWA NA MAMA RAIA WA CZECH HUKU BABA YAKE AKITOKEA ETHIOPIA

REKODI MCHEZO WA UFUNGUZI ULAYA 2012


Kuelekea mchezo wa ufunguzi michuano ya ulaya 2012 kati ya Poland dhidi ya Ugiriki rekodi ambazo zinasimama hadi sasa kwa timu hizo mbili ambapo hadi sasa wameshakutana mara 15 huku Poland ikishinda mara 10, suluhu 2, wakipoteza 3.
1. Lakini katika rekodi hizo Poland imefunga magoli 29 dhidi ya 11 ya Ugiriki.
2. Katika mechi 5 zilizopita Poland imeshinda mechi 4 huku wakicheza bila kufungwa, mara ya mwisho Ugiriki kuifunga Poland kwenye mechi za mashindano ni 1987 jijini Athens kwenye michuano ya Ulaya kwa ushindi wa 1-0 kwa goli la dakika ya 57 la Dimitris Saravakos.
3. Ugiriki imefungwa mechi zote 8 ambazo imecheza na Poland ugenini wakifunga magoli 4 na kuruhusu magoli 22.
4. 29th MEI, 2004 Poland waliishinda Ugiriki kwa goli 1-0 baada ya Michalis Kapsis kujifunga mwenyewe kwenye michuano ya Ulaya.
5. 12th AGOSTI, 2009 Poland walishinda kwa magoli 2 -0 dhidi ya Ugiriki kupitia kwa Ludovic Obraniak akiingia kama mchezaji wa akiba kipindi cha pili.
6. 29th MACHI, 2011 timu hizi zilikutana kwenye uwanja wa Georgios Karaiskakis mchezo ukimalizika kwa suluhu ya
0-0   
Ugiriki: Chalkias, Vyntra, Moras, Papadopoulos, Lagos, Kone (Liberopoulos 67), Kafes, Karagounis (Katsouranis 73), Fetfatzidis (Torossidis 77), Mitroglou (Ninis 58), Samaras (Salpingidis77). 
Poland: Sandomierski, Piszczek, Żewłakow (Jodłowiec 63), Głowacki, Sadlok, Mierzejewski (Murawski 46), Dudka, Obraniak (Roger Guerreiro 83), Błaszczykowski, Peszko (Grosicki 77), Lewandowski (Kucharczyk 83).

KUYT KUTIMKIA UTURUKI

Klabu ya soka ya Liverpool maarufu kama majogoo wa jiji imeamua kumwachilia mshambuliaji wake raia wa Uholanzi, Dirk Kuyt(pichani) mwenye miaka 31 baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu 6 akitokea Feyernoord ya Uholanzi.
Kuyt anatarajiwa kujiunga na Fernabahce ya Uturuki siku chache zijazo  kulingana na taarifa za mtandao wa klabu ya Liverpool, ambao hivi karibuni imemsajili kocha mpya, Brendan Rogders kutoka Swansea City.
Kuyt ambae anajiandaa na michuano ya Ulaya inayofanyika nchini Poland na Ukraine alijiunga na Liverpool 2006 akitokea Feyernoord ya Uholanzi akicheza mechi 285 na magoli 71 ikiwemo matatu (hat trick) dhidi ya Manchester United msimu ulipita.
Kuyt pia alifunga goli mojawapo kwenye mchezo wa fainali ya kombe la ligi mwezi Februari dhidi ya Cardiff City kwenye uwanja wa Wembley.

ONYANGO, MWESIGWA KUIONGOZA UGANDA DHIDI YA ANGOLA


Kocha wa timu ya taifa ya Uganda ‘the cranes’ raia wa Scotland, Sir Bobby Williamson ameteua kikosi kitakachoanza hii leo kwenye mchezo wao na Angola mjini Luanda hapo kesho kikiongozwa na nyota kama Denis Onyango na Andy Mwesigwa kwenye kundi J.

Kikosi kamili:

Denis Onyango; Simeon Masaba, Godfrey Walusimbi, Andy Mwesigwa, Hassan Wasswa; Dan Wagaluka, Tonny Mawejje; Johnson Bagoole, Mike Sserumaga, Martin Mutumba; Emmanuel Okwi.

Wachezaji wa akiba: Hamza Muwonge, Denis Guma, Henry Kalungi, Habib Kavuma, Patrick Ochan, Moses Oloya, Fabian Kizito

Mfumo :4-2-3-1

Mara nne za mwisho kukutana kati ya Uganda and Angola

04.09.2011 -  Angola 2-0 Uganda

04.09.2010 –  Uganda 3-0 Angola

23.06.2008 –  Angola 0-0 Uganda

14.06.2008 –  Uganda 3-1 Angola


MATOKEO MECHI ZA KIMATAIFA


Mechi za kirafiki za kimataifa
Portugal

 1 - 3
Turkey
Lisbon
Netherlands
6 - 0
Northern Ireland
Amsterdam
Norway
1 - 1
Croatia
England
1 - 0
Belgium
Wembley
Poland
4 - 0
Andorra
Warsaw
Denmark
2 - 0
Australia
Copenhagen
Mechi za kufuzu kombe la dunia 2014 Brazil – Ukanda wa Afrika
Algeria
4 - 0
Rwanda
Blida
Burkina Faso
0 - 0
Congo
Ouagadougou
Senegal
3 - 1
Liberia
Dakar
Sudan
2 - 0
Zambia
Khartoum
Ivory Coast
2 - 0
Tanzania
Abidjan
Tunisia
3 - 1
Equatorial Gine
Monastir
Sierra Leone
2 - 1
Cape Verde
Freetown
Gambia
1 - 1
Morocco
Bakau
Cameroon
1 - 0
Congo DR
Yaounde
Central African Republic
2 - 0
Botswana
Bangui
Kenya
0 - 0
Malawi
Nairobi
Mechi za kufuzu kombe la dunia 2014 Brazil – Ukanda wa Amerika Kusini
Bolivia
0 - 2
Chile
La Paz
Uruguay
1 - 1
Venezuela
Montevideo