VIEW OTHER SITES

Saturday

NYOTA ATLETICO ANAYENG'ARISHA MCHEZO WA STARS DHIDI YA THE FLAMES


JINA: ROBIN NGALANDE
TAREHE YA KUZALIWA: NOVEMBA, 2, 1992.
TAIFA: MALAWI.
KLABU: ATLETICO DE MADRID, UHISPANIA (MKOPO)
NAFASI: MSHAMBULIAJI.
UREFU: 1.70 M (5ft7 in)
MWAKA           TIMU
2009            CIVO UNITED, MALAWI
2009 -2010      MAMELODI SUNDOWNS, AFRIKA KUSINI.
2010 -          ATLETICO DE MADRID, UHISPANIA.
TIMU YA TAIFA
MWAKA     TIMU     MECHI    MAGOLI
2010 -    MALAWI     1       0

Ngalande yupo chini ya Sport Agency kampuni ambayo pia ni wakala wa Benni McCarthy, amecheza mechi moja ya kimataifa na timu ya Malawi “The Flames” mnamo Julai,6, 2010 kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa nchi hiyo dhidi ya Lesotho iliyopigwa uwanja wa Civo uliopo mji mkuu wa nchi hiyo, Lilongwe.
Mwaka 2010 alishiriki michuano ya vijana U-18 nchini Uhispania akiwa na kikosi cha vijana cha Sondowns huku akifunga magoli mawili kwenye mechi tatu, kabla ya kutolewa hatua ya robo fainali na Boca Junior ya Argentina.
Miongoni mwa vilabu vilivyowahi kumtaka kinda huyo wa Malawi ni pamoja na Chelsea, Manchester City na Espanyol.