VIEW OTHER SITES

Monday

KAMATI YA UCHAGUZI TFF YATOA AGIZO KWA YANGA

Kikao cha kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake, Deogratias Lyatto kimejadili mustakabali wa nafasi za uongozi ndani ya klabu ya Yanga kufuatia kujiuzuru kwa wajumbe nane na mmoja kufariki dunia kati ya wajumbe 13, hivyo kutoa ufafanuzi na kuipa maagizo Kamati ya Uchaguzi ya Yanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipokea ushauri wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF na kutoa ufafanuzi na maagizo yake ikiwemo kuitaka Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuanza mchakato wa kujaza nafasi za wazi za Kamati ya Utendaji kwa mujibu wa Katiba ya Yanga Ibara ya 28.
Mchakato huo umetakiwa kuanza mapema  Juni mosi na Julai 15 uchaguzi ufanyike kuziba nafasi zilizoachwa na wajumbe walijuizuru baada ya kupangwa mahali pa kufanyia uchaguzi huo na Kamati ya Uchaguzi wa Yanga kwa kushirikiana na Sekretariati ya Yanga.
Vile vile Kamati ya Uchaguzi ya TFF imesisitiza kuwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi uwe na ajenda moja tu ya Uchaguzi ili kujaza nafasi za wazi za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga.
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliobaki kwenye nafasi zao hadi sasa ni Sarah Ramadhan, Mohamed Bhinda, Tito Osoro na Salim Rupia.

No comments:

Post a Comment