Bingwa wa zamani wa mita 10,000 duniani raia wa Ethiopia, Haile Gebrselassie ameshindwa kufuzu kwa mashindano ya Olimpiki ya London, Uingereza baada ya kushika nafasi ya saba kwenye mashindano ya Fanny Blankers-Koen yaliyofanyika Hengelo, Uholanzi.
Gebrselassia mwenye miaka 39 alimaliza mbio hizo kwa dakika 27 na sekunde 20.39 huku mshindi Tariku Bekele kutoka Ethiopia akitumia dakika 27 sekunde 11.70 katika mashindano hayo yaliyoandaliwa maalumu ili kupata wawakilishi wa Ethiopia kwenye mashindano ya Olimpiki.
Wanariadha wengine waliungana na Bekele ni Leleisa DEsisa Benti aliyeshika nafasi ya pili, huku nafasi ya tatu ikienda kwa Kenenisa Bekele.
Gebrselassie mshindi wa mbio za Great Manchester wiki iliyopita ameshindwa kufuzu kwa mashindano yake ya tano ya Olimpiki huku akifanikiwa kushinda medali za dhahabu mwaka 1996 na 2000 mbio za mita 10,000.
Matokeo mengine,
Wanaume
100m (0.5 m/s)
1. Churandy Martina (NED) 10.18
2. Mario Forsythe (JAM) 10.25
3. Ainsley Waugh (JAM) 10.31
400m:
1. Luguelin Santos (DOM) 44.45
2. Martyn Rooney (GBR) 44.97
3. Nery Brenes (CRC) 45.20
5. Oscar Pistorius (RSA) 46.35
800m:
1. Adam Kszczot (POL) 1:43.83
2. Timothy Kitum (KEN) 1:44.00
3. Job Kinyor (KEN) 1:44.17
1500m:
1. Nixon Chepseba (KEN) 3:29.90
2. Ayanleh Souleiman (DJI) 3:30.31
3. Mekonnen Gebremedhin (ETH) 3:31.45
10000m:
1. Tariku Bekele (ETH) 27:11.70
2. Leleisa Benti (ETH) 27:11.98
3. Sileshi Sihine (ETH) 27:12.60
7. Haile Gebrselassie (ETH) 27:20.39
110m hurdles:
1. Ronnie Ash (USA) 13.31
2. Andrew Pozzi (GBR) 13.39
3. Arthur Noga (POL) 13.45
Wanawake
200m:
1. Charonda Williams (USA) 22.73
2. Jamile Samuel (NED) 22.93
3. Tiffany Towsend (USA) 23.04
800m:
1. Janeth Jepkosgei (KEN) 1:57.79
2. Yuneysi Santiusti (CUB) 1:58.53
3. Annet Negesa (UGA) 1:59.08
1500m:
1. Hanna England (GBR) 4:04.05
2. Corina Harrer (GER) 4:04.81
3. Laura Weightmann (GBR) 4:04.88
100m hurdles:
1. Kellie Wells (USA) 12.81
2. Lolo Jones (USA) 12.90
3. Queen Harrison (USA) 12.98
Discus
1. Zaneta Glanc (POL) 64.71m
2. Sendriute Zinaida (LIT) 62.74
3. Joanna Wisnewska (POL) 59.50
No comments:
Post a Comment