VIEW OTHER SITES

Monday

ITALIA YAINUSURU UJERUMANI NA DHAHAMA YA MWAKA


                                 KIUNGO WA ITALIA, ANDREA PIRLO AKIKABILIANA NA 
KIUNGO WA UHISPANIA, SERGIO BOSQUETS KWENYE
MCHEZO WA FAINALI HAPO JANA UHISPANIA 
ILISHINDA KWA MAGOLI 4 -0 . 

 ANDRES INIESTA LUJAN "MAESTRO" AKIWATOKA VIUNGO
WA ITALIA.

 KIUNGO MSHAMBULIAJI WA UHISPANIA, DAVID SILVA(21)
AKIFANYA VITU VYAKE MBELE YA  EMANUELE GIACCHERINI(13)
HAPO JANA  KWENYE MCHEZO WA FAINALI.

 BALOTELLI CHINI YA ULINZI WA SERGIO RAMOS KWENYE
MCHEZO WA FAINALI KATI YA UHISPANIA DHIDI YA ITALIA JANA. 

 MASHABIKI WA UHISPANIA WAKISHANGILIA USHINDI WAO
HUKU WENGINE WAKIWA HAWAAMINI KILICHOTOKEA 
BAADA YA UHISPANIA KUSHINDA KWA MAGOLI 4-0, IKIFUTA
REKODI YA KUTOIFUNGA ITALIA NDANI YA DAKIKA TISINI TANGU
MWAKA 1920. 

 MFUNGAJI BORA WA MICHUANO YA ULAYA "EURO2012" 
FERNANDO TORRES AKISHANGILIA BAADA YA KUIFUNGA 
ITALIA HAPO JANA.

MASHABIKI WA ITALIA BAADA YA MCHEZO WA FAINALI
DHIDI YA UHISPANIA KUMALIZIKA KWA ITALIA KULALA
KWA MAGOLI MANNE BILA MAJIBU. 
 
 SEHEMU YA MASHABIKI WA UHASPANIA JIJINI MADRID
UHISPANIA HAPO JANA BAADA YA TIMU YAO KUTWAA
UBINGWA WA ULAYA KWA MARA YA PILI MFULULULIZO
BAADA YA KUFANYA HIVYO MWAKA 2008. 

TWIGA STARS YAIBUA MAPYA


Uongozi wa Twiga Stars umekana kuwepo vitendo vya kinyume na maadili kwa wachezaji wa timu hiyo ambayo hivi karibuni ilitolewa kwenye mechi za mchujo za michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC).
Wakizungumza na waandishi wa habari leo, Meneja wa Twiga Stars, Furaha Francis na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa wamesema hakuna vitendo vya aina hiyo.
Mkwasa amesema alikaririwa vibaya kuhusu suala hilo wakati akiwa kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha Star Tv kutokana na swali alilokuwa ameulizwa kuhusiana na vitendo hivyo.
“Ukifuatilia mahojiano yangu na Star Tv mimi sikusema kuwa kuna vitendo hivyo. Tatizo nadhani lilianzia kwa magazeti yaliyonukuu kupitia Star Tv, na wala kujiuzulu kwangu hakukuhusiana na hilo, nimewajibika kama kocha kutokana na kutolewa na Ethiopia,” amesema Mkwasa.
Naye Furaha Francis amesisitiza kuwa hakuna vitu vya aina hiyo katika timu hiyo, na kama kuna mtu ana ushahidi na hilo ni bora akauonesha badala ya kuzungumzia uvumi kuliko ukweli.
“Ukweli ni kwamba si sisi na wachezaji tu ambao hatukufurahishwa kutolewa na Ethiopia, wapo Watanzania wengi ambao hawakufurahishwa na matokeo yale. Twiga Stars si timu ya kudumu, haikai na wachezaji kwa muda wote, kila mchezaji ana timu yake.
“Madai yanayoenezwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu vitendo hivyo yametuchafua sana. Tunaomba kama kuna mtu ana ushahidi na hilo atueleze kuliko kuendelea kutuchafua,” amesema.

NIYONZIMA AREJEA JANGWANI


Kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima "Fabregas" amerejea jana usiku na kujiunga na kikosi cha Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Young Africans Sport Club (YANGA) katika mazoezi yaliyotarajiwa kuanza leo jioni saa kumi katika uwanja wa Kaunda Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na tovuti ya klabu www.youngafricans.co.tz kiungo huyo amesema kuchelewa kwake kulitokana na matatizo binafsi yaliyomkuta wakati akiwa nchini kwao na kusababisha kuchelewa kujiunga na Kikosi chake.

Haruna amewataka wachezaji wenzake kurejesha heshima kwa mara nyingine kwa kutwaa kombe la Kagame katika michuano inayotarajiwa kuanza Julai 14 Mwaka huu, huku Yanga ikiwa ndiyo Mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

Niyonzima amesema tangu alipokuwa mapunziko alikuwa akifuatilia kwa karibu juu ya Klabu yake ya Yanga hasa katika zoezi la usajiri unaoendelea na kupongeza usajili huo kutokana na baadhi ya wachezaji anaowafahamu kusajiriwa katika kikosi hicho.

Yanga itaanza kutupa karata yake dhidi ya Atletico ya Burundi ambapo mechi hiyo ndiyo itakayokuwa ni pekee wakati wa ufunguzi itachezwa katika uwanja wa Taifa,Jijini Dar es Salaam huku Simba ikaanza kampeni siku inayofuata.

Mabingwa hao watetezi kundi lake limejumuisha na timu za Wau Salaam ya Sudan,Altetico ya Burundi na APR ya Rwanda.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa BARAZA la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholous Musonye amesema mpaka sasa mdhamini ni mmoja aliyejitosa kwenye michuano hiyo ambaye ni Rais wa Rwanda,Paul Kagame.

Jumla ya timu 12 zitashiriki katika michuano hiyo ambayo itaanza Julai 14 hadi Julai 28 ambapo wawakilishi hao watatoka katika nchi za Tanzania,Uganda,DR Congo,Djibout,Zanzibar,Kenya,Sudan Kusini,Rwanda na Burundi.(Mwandishi wetu Louis Sendeu)

RUVUMA YAISAFISHA LINDI MKOANI PWANI


Timu ya mkoa wa Ruvuma(U-17) imefanya kweli hii leo katika michuano ya Copa Coca-Cola baada ya kuishushia Lindi kipigo cha mabao 7-2 asubuhi ya leo.
Mechi hiyo ya kundi A iliyochezwa Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani, washindi ambao kwa matokeo hayo wamejiweka katika nafasi nzuri ya kucheza 16 bora walikuwa mbele kwa mabao 3-0.
Waliotikisa nyavu ni Anthony Christian dakika ya 23 na 50, Edward Songo dakika ya 27, 75 na 86 na Sunday Leonard dakika ya 32 na 60. Mabao ya Lindi yalifungwa na Salum Mnyamwile dakika ya 18 kwa njia ya penalti na lingine dakika ya 48 kupitia kwa Mwarami Maundu.
Nayo Tanga imepata ushindi wake wa kwanza katika michuano hiyo baada ya kuifunga Manyara mabao 2-0 katika mechi ya kundi B iliyochezwa Uwanja wa Tamco mkoani Pwani. Mabao ya washindi yalifungwa na Mbwana Musa dakika ya 47 na Issa Mwanga dakika ya 60.
Tanga ilitoka sare ya mabao 3-3 na Morogoro, ikapata sare nyingine ya 1-1 dhidi ya Mwanza.
Kagera imeendelea kujitutumua katika michuano hiyo baada ya kupata ushindi wake wa pili katika kundi D kwa kuilaza Kusini Unguja bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe jijini Dar es Salaam.
Bao lake lilifungwa dakika ya 76 na Novati Sebastian. Mechi iliyopita Kagera iliifunga Tabora mabao 2-0 baada ya kuteleza katika mechi mbili za kwanza kwa kufungwa na Kilimanjaro na Singida.
Mechi nyingine ilichezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambapo Kinondoni iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mara.

MAKUNGU AUTWAA URAIS ZFA


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) linampongeza Amani Ibrahim Makungu kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) katika uchaguzi uliofanyika juzi (Juni 30 mwaka huu) kwenye hoteli ya Bwawani, mjini Zanzibar.
Ushindi wa asilimia 94 alioupata Makungu ambaye hakuwa na mpinzani katika uchaguzi huo mdogo unaonesha imani ambayo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA wanayo kwake katika kukiongoza chama hicho.
Ni matarajio ya TFF kuwa ushindi huo utatafsiriwa kwa vitendo na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA na wadau wa mpira wa miguu Zanzibar kwa kumpa Makungu ushirikiano wa asilimia 100 ili kuhakikisha Kamati yake ya utendaji inafanya kile kinachotarajiwa na wengi.
Makungu si mgeni katika mpira wa miguu, na mchango aliotoa kwa mchezo huo visiwani kabla ya kuwania nafasi hiyo unatambuliwa na kila anayefuatilia maendeleo ya mpira wa miguu katika Zanzibar.
TFF tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa ZFA chini ya Makungu kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Ali Ferej Tamim ili kuhakikisha ustawi wa mpira wa miguu visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Makungu pia amepata kuwa mfadhili wa klabu ya Miembeni ya visiwani humo.