VIEW OTHER SITES

Wednesday

UJUZI NA UFUNDI WA RAFAL WOLSKI

MAXIMO KUTUA BONGO KUIFUNDISHA YANGA


Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Mbrazili Marcio Maximo amewasili nchini ili kumalizia mazungumzo yao ya kuingia mkataba na klabu ya Young Africans “Yanga” kuifundisha kwa msimu ujao.
Yanga ambao wameamua kukutana na kocha huyo baada ya kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa klabu hiyo, Mserbia Konstadin Papic ambaye aliondoka mwishoni mwa msimu uliopita kuelekea kwao.
Maximo alikuwa na Stars kutoka 2006 hadi 2010 mkataba wake ulipomalizika kabla ya Mdenimaki Jan Poulsen kuchukua nafasi yake.
Mwaka 2009 aliiwezesha Tanzania kushiriki mashindano ya afrika wa wachezaji wa ndani yaliyofanyika nchini Ivory Coast.
Yanga ambayo inatarajiwa kufanya uchaguzi wake mnamo Juni 17 imemaliza nafasi ya 3 kwenye ligi kuu ya Vodadom msimu huu, inatarajiwa kushiriki mashindano ya Afrika Mashariki na Kati baadaye mwaka huu pekee kwenye medani ya kimataifa ikiingia kama bingwa mtetezi.

MILITO ATUNDIKA DARUGA


Beki wa zamani wa Argentina, Gabriel Alejandro Milito ametangaza kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu baada ya kudumu kwa miaka 15  akiwa na vilabu tofauti barani Amerika ya Kusini na Ulaya.
Milito mwenye miaka 31 ambaye pia ni ndugu wa Mshambuliaji wa Inter Milan, Diego Milito amechezea vilabu mbalimbali ikiwemo FC Barcelona, Real Zaragoza na sasa akiwa na Independiente kama nahodha wa klabu hiyo.
Milito ameanza soka lake na Independiente akiwa na mika 17 mwishoni mwa mwaka 1997 hadi 2003 alipohamia Zaragoza ya Uhispania akicheza kwa misimu minne ya mafanikio kabla hajasaini na Barcelona 2007 ambapo aliachana nayo mwaka 2011.
Amepata kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina kwenye michezo 42 ikiwemo kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani.
Milito amezaliwa Septemba 7, 1980 jijini Bernal, Argentina.
MATAJI ALIYOTWAA;
Independiente 
Argentine League: (1) Apertura 2002

Zaragoza
Kombe la Uhispania: (1) 2004

Barcelona
Ligi ya Uhispania(3): 2009, 2010, 2011
Kombe la Uhispania (1): 2009
Klabu bingwa Ulaya(2): 2009, 2011

METODO; MFUMO WA KIITALIANO ULIOHAMISHIWA BARCELONA NA GUARDIOLA

 
Mfumo huu ulioasisiwa na kocha wa timu ya taifa ya Italia, Vittorio Pozzo miaka ya 1930 ambapo mabeki wa kati wanasaidia viungo huku mabeki wa pembeni wakiwa na jukumu kubwa la kusaidia mashambulizi kutokea pembeni. Italia ilitumia mfumo huo kwenye kombe la dunia 1934 na 1938. Pia, Pep Guardiola alitumia mfumo huo akiwa na Barcelona ukiwa umeboreshwa zaidi.

  VITTORIO POZZO








 KIKOSI CHA ITALIA MWAKA 1934 KIKIWA UWANJANI KABLA YA KUWAKABILI JAMHURI YA CZECH KIKIONGOZWA NA NYOTA, Giuseppe De Meazza.

MWINYI MGENI RASMI TUZO ZA TASWA


RAIS mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya pili, Alhaji Ally Hassan Mwinyi, amechaguliwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za utoaji tuzo za wanamichezo bora Tanzania zitakazofanyika hapo kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Abbas Pinto amesema hayo kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari mchana huu katika ukumbi wa City Sports Lounge, jijini Dar es Salaam na kwamba wamemchangua Mwinyi kwa sababu alikuwa ana mchango mkubwa katika sekta ya michezo enzi zake, akiwa Ikulu tangu 1985 hadi 1995 alipomuachia Benjamin William Mkapa.
Katika tuzo hizo, kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Fadhil Hakizimana Niyonzima wa Yanga, atachuana na Kipre Tchetche wa Ivory Coast anayechezea Azam FC na Mganda Emmanuel Okwi wa Simba kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa mwaka wa kigeni.
Kwa upande wa wanasoka wazalendo, tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka inawaniwa na John Bocco, Aggrey Morris, wote wa Azam na Juma Kaseja wa Simba, wakati kwa wachezaji wa Tanzania wanaocheza nje wanaoshindana ni Henry Joseph wa Kongsvinger ya Norway na Mbwana Samatta wa Tout Puissant Mazembe ya DRC.
Kwa upande wa wanawake, Sophia Mwasikili anayecheza Uturuki, anashindana na Asha Rashid ‘Mwalala’, Mwanahamisi Omary wote wa Mburahati Queens, Fatuma Mustapha wa Sayari na Eto’o Mlenzi wa JKT.
Tuzo hizo zinadhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).