Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetoa tahadhari kwa shirikisho la soka nchini Kenya kusimamia usalama wa mchezo wake na Malawi utakaofanyika wikendi hii uwanja wa Nyayo.
Mchezo huo ni wa mchujo ili kupata nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014 ambapo Kenya itacheza na Malawi Juni 2 mwaka huu.
FIFA imetoa tahadhari hiyo kufuatia vitendo vya ulipuaji mabomu vinavyofanyika kwenye nchi huku kundi la kigaidi kutoka nchini Somalia, Al-Shabaab likihusishwa na mashambulio hayo.
Mwaka jana FIFA waliufungia uwanja wa Nyayo kutokana na kuingiza watu zaidi ya idadi inayotakiwa vurugu baina ya mashabiki, hivyo kulitaka shirikisho kusimamia utulivu na usalama ili kuepuka kufungiwa kufanyika kwa mchezo wowote wa kimataifa nchini humo.
No comments:
Post a Comment