VIEW OTHER SITES

Monday

ZESCO YAENDELEA KUONGOZA LIGI KUU ZAMBIA


Klabu ya Zesco United imefanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini Zambia baada ya kuifunga National Assembly kwenye uwanja wa Mwanawasa kwa 1-0 wakifikisha alama 27 kwa ushindi huo.
Zesco walipata ushindi wao kupitia kwa Kondwani Mtonga ikiunganisha krosi ya Innocent Mwiba dakika ya 75 akiwazidi ujanja mabeki wa National Assembly kuifanya tiu hiyo kuweka wigo wa alama nne mbele ya Zanaco yenye alama 23.
Hata hivyo Zesco walikosa nafasi ya wazi dakika ya 6 wakati Alfred Luputa akipiga krosi ambayo ilimshinda mlinda mlango wa National Assembly, Phillip Banda lakini washambuliaji wa Zesco wakikosa umakini kumalizia krosi hiyo.
Mchezo huo pia ulishuhudiwa kwa kocha wa Zesco, Wedson Nyirenda alipewa kadi nyekundu baada ya kumtolea mwamuzi, Joseph Jere maneno machafu kufuatia mchezo mbaya aliofanyiwa Jackson Mwanza.

No comments:

Post a Comment