VIEW OTHER SITES

Saturday

MEDALI OLIMPIKI HADI SASA

MEDALI MASHINDANO YA OLIMPIKI 
DHAHABU(D) FEDHA(F) NA SHABA(S)
1United States United States 22 (D)10 (F)13(S)  45(JUMLA)
2China China 20 14 9 43
3Great Britain Great Britain 10 7 8 25
4Korea Korea 9 2 5 16
5France France 8 5 6 19
6Germany Germany 5 9 6 20
7Italy Italy 4 5 3 12
8DPR Korea DPR Korea 4 0 1 5
9Kazakhstan Kazakhstan 4 0 0 4
10Russian Fed. Russian Fed. 3 12 9 24
11South Africa South Africa 3 1 0 4
12New Zealand New Zealand 3 0 4 7
13Japan Japan 2 8 11  21
14Cuba Cuba 2 2 1 5
15Netherlands Netherlands 2 1 3 6
16Hungary Hungary 2 1 2 5
17Poland Poland 2 1 1 4
18Ukraine Ukraine 2 0 4 6
19Australia Australia 1 10 6 17
20Romania Romania 1 4 2 7         

OLIMPIKI HADI FAINALI SOKA WANAUME

ROBO FAINALI
MECHISIKU                - MUDAUWANJA


2504/08 13:00Manchester Japan3:0 (1:0)Egypt
2604/08 15:30London Mexico
Inaendelea
Senegal
2704/08 18:00Newcastle BrazilHonduras
2804/08 20:30Cardiff Great BritainKorea Republic
NUSU FAINALI
MECHISIKU - MUDAUWANJA


2907/08 18:00London
W26 - Japan
3007/08 20:45Manchester
W28 - W27
MECHI YA MEDALI YA SHABA
MECHISIKU- MUDAUWANJA


3110/08 20:45Cardiff
L30 - L29
MECHI YA MEDALI YA DHAHABU
MECHISIKU -MUDAUWANJA


3211/08 16:00London
W30 - W29

JAPAN YATANGULIA NUSU FAINALI

Japan Misri

JapanEgypt
3:0

  • Kensuke NAGAI (14')
  • Maya YOSHIDA (78')
  • Yuki OTSU (83')


Japan first to reach semi-finals

Vikosi


1
Shuichi GONDA (GK)
1
(GK) Ahmed ELSHENAWI
2
Yuhei TOKUNAGA Yellow Card
5
(C) Mohamed ABOUTRIKA
3
Takahiro OHGIHARA
6
Ahmed HEGAZI
4
Hiroki SAKAI
7
AHMED FATHI
5
Maya YOSHIDA (C) Goal
8
Out (-45'+1 ) Shehab AHMED
7
Yuki OTSU Goal
10
Out (-74' ) EMAD METEAB
10
Keigo HIGASHI Out (-72' )
11
Out (-58' ) MOHAMED SALAH
11
Kensuke NAGAI Goal Out (-20' )
12
Eslam RAMADAN
13
Daisuke SUZUKI
14
HOSSAM HASSAN
16
Hotaru YAMAGUCHI
15
Red Card Saadeldin SAAD
17
Hiroshi KIYOTAKE Out (-84' )
17
Mohamed EL NENY

Wachezaji wa Akiba

6
Taisuke MURAMATSU
2
Yellow Card In (+45'+1) Mahmoud ALAA ELDIN
8
Kazuya YAMAMURA
3
ALY FATHY
9
Kenyu SUGIMOTO
4
In (+58') OMAR GABER
12
Gotoku SAKAI In (+72')
9
In (+74') Marwan MOHSEN
14
Takashi USAMI In (+84')
13
SALEH GOMAA
15
Manabu SAITO In (+20')
16
Ahmed MAGDY
18
Shunsuke ANDO
18
Mohamed BASSAM

Makocha

Takashi SEKIZUKA (JPN)
(EGY) Hany RAMZY

FA ZAMBIA YAFANYA MABADILIKO TIMU ZA VIJANA

Kocha wa Konkola Mine Police, Masauso Mwale anachukua nafasi ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanawake akisaidiwa na Enala Simbeye Phiri na Kaluba Kangwa. Wengine ni Besa Chibwe meneja wwa timu, Dorothy Mabomahoko na Cornelia Chazura wanakuwa daktari na mtaalamu wa mifupa.
Timu ya taifa ya wanawake ya chini ya miaka 17 kocha mkuu kuwa, Albert Kachinga akisaidiwa na Masiye Mukwasa na Kape Saili. Meneja wa timu kuwa, Clementina Mazuba, wakati Womba Kadochi anakuwa daktari wa timu na Chabu Bwalya kuwa mtaalamu wa mifupa.
Timu ya chini ya miaka 20, kocha mkuu kuwa, Chris Kaunda lakini kabla Kaunda alikuwa kocha mkuu wa timu ya chini ya miaka 17 na sasa atafanya kazi na kocha wa sasa wa Zanaco, Keegan Mumba na kocha msaidizi wa Power Dynamos, Hector Chilombo.
Lighton Ndashe wa Lime Hotspurs ameteuliwa kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya wanaume cha chini ya miaka 20 cha Zambia akichukua nafasi ya Stanley Kaseko ambaye anachukua nafasi nyingine kwenye timu ya taifa ya wakubwa "Chipolopolo" wakati Daktari George Magwende na Peter Phiri wanaendelea kuwa matabibu wa timu hiyu.
Nayo timu ya U17 ya wanaume itakuwa na kocha msaidizi wa Green Buffaloes’ Bilton Musonda hkama kocha msaidizi wa U17 wanaume. Osward Mutapa anabakia kama kocha mkuu huku kocha wa zamani wa Nkana, Linos Makwaza akiwa msaidizi wake. Daniel Jere atabakia kama meneja wa timu hiyo.

KENYA U17: 20 WATEULIWA NA FKF





SHIRIKISHO la SOka nchini Kenya (FKF) limeteua wachezaji 20 watakaounda kikosi cha timu ya taifa U17 kitakachoikabili Tanzania ili kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17.
Wachezaji hao hao wanatarajiwa kufanyiwa vipimo vya MRI ili kutambua miaka yao sahihi likiwa ni agizo la shirikisho la soka barani afrika (CAF).
Wachezaji hao wanatokana na michuano ya Copa Coca Cola na mashindano ya vijana nchini humo.
Kwa upande mingine FKF imeandaa mechi za kirafiki kwa timu dhidi ya timu za majimbo, mataifa mengine pamoja na klabu za ligi kuu nchini humo kabla kuingia kambini Agosti 20 kwa ajili ya mafunzo.
Timu hiyo iko chini ya Kocha mkuu David Ouma na wasaidizi wake, Eliud Omukuiya na Kinero Swaleh, huku Jabir Hassan akiwa mkufunzi wa makipa na meneja wa timu ni Sammy Okoth.
Kikosi kamili kinaundwa na Omar Musa, Isaack Aliwa, Eugine Moses, Stephen Ogweno, Apolo Otieno, James Mazembe, Sylvester Godwin, Ibrahim Moge, Alfred Wekesa, Eugine Chege, Castro Mwaura, Robert Mutua, Boniface Mwenda, Kelvin Otieno, Peter Mwaguna,Shaubi Rashid, William Waithaka, Oruchum Christopher, Edwin Mukolwe, Moses Mwangi.

RED BULL YAMSIKILIZIA OKWI

Klabu ya FC Red Bull Salzburg ya nchini Austria wenda ikasitisha mpango wake wa kumsajili mshambuliaji wa Simba SC na timu ya taifa ya Uganda, Emmanuel Arnold Okwi, licha kufuzu majaribio katika klabu hiyo kwa wiki tatu alizokuwa nchini humo akifanyiwa majaribio.
Habari kutoka Simba SC zimesema kuwa, Okwi amekwama na anarejea Simba SC, huku kukiwa na uvumi unaomhusisha mshambuliaji huyo wa zamani wa SC Villa ya Uganda na kuelekea mtaa wa Jangwani ikiwa ni mipango ya uongozi mpya wa Yanga kuimarisha safu ya ushambuliaji.
Kwa sasa Okwi yuko nchini Uganda kutoka Austria, kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa Malaria.
Hata hivyo Katibu wa Simba Evodius Mtawala amesema kuwa; “Okwi amefuzu majaribio, ila ana Malaria, amekuja kuitibu kisha atarudi Austria kwa ajili ya vipimo,”alisema Mtawala.
Klabu hiyo ya Austria ilipanga kuipa Simba SC Euro 600,000,
Hapo kabla, Simba ilipata ofa ya Sh. Bilioni 2 kutoka kwa miamba ya soka ya Afrika Kusini, Mamelodi Sundown lakini mshambuliaji huyo hakuwa tayari kujiunga na klabu hiyo.
Lakini pia, Olando Pirates ya Afrika Kusini ilimuomba Okwi akafanye majaribio huko kama angefuzu wangemsajili dau la dola 550,000 kabla ya kuibuka kwa taarifa za kutakiwa na klabu ya Parma ya Italia.

MANJI KUANZA KAZI RASMI KESHO

Hapo kesho majira ya saa 4:00 asubuhi, uongozi mpya wa klabu ya soka ya  Yanga utaingia rasmi kwa kuapishwa na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini, Mama Fatuma Karume kwenye makao makuu ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam.
Kisha wachezaji na viongozi wa Yanga wataelekea mkoani Dodoma kufuatia mwaliko wa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wapenzi wa klabu hiyo siku ya Jumatatu.
Mwaliko huo unatokana na kulitwaa taji la klabu bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati,Kagame, Jumamosi iliyopita, wakiifunga Azam FC mabao 2-0 kwenye fainali, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Julai 15, mwaka huu, Yanga ilipata uongozi mpya chini ya uenyekiti wa, Yussuf Manji, Makamu wake akiwa, Clement Sanga na wajumbe wanne wa kamati ya utendaji, Abdallah Bin Kleb, George Manyama na Mussa Katabaro.
Wajumbe wengine waliosalia kutoka uongozi uliopita, Mohamed Bhinda, Titto Osoro, Salim Rupia na Sarah Ramadhan baada ya wajumbe wengine, wakiwemo Mwenyekiti, Wakili Lloyd Nchunga na Makamu wake, Davis Mosha kujiuzulu.