VIEW OTHER SITES

Thursday

AHMED HASSAN NA MISRI KUJIFUNGIA NA MSUMBIJI


Cafonline.com: Unautazamaje mchezo wa Ijumaa(Leo) dhidi ya         Msumbiji?
 
Hassan: Utakuwa mgumu. Kwanza mara nyingi wamekuwa wagumu hasa mechi za kufuzu. Na hali ya sasa inaufanya kuwa mgumu zaidi maana tunacheza milango ikiwa imefungwa na tunakosa soka la haswa kutokana na hali ya amani Misri. Ila tunatazamia kupata ushindi.
 
Cafonline.com: Unalizungumziaje kundi lenu mkiwa na Msumbiji, Guinea na Zimbabwe?

Hassan: Tunaziheshimu timu zote bila kuangalia majina yao. Soka la Afrika limekuwa sana kwa ubora bila kujali nchi. Mwaka huu tulipoteza dhidi ya Niger, Sierra Leone mbali na kuwa chini sana kwa ubora ukilinganisha na sisi wakati huo.
 
Cafonline.com: Unadhani mtaathirika kucheza bila mashabiki wenu?

Hassan: Tunatumaini mambo yatabadilika Misri na tutakuwa na mashabiki wetu. Lakini kwa sasa tunakubali kucheza bila mashabiki kutokana na hali ya usalama. Naamini hatutaathirika kwa kiwango kikubwa kutokana na kuwakosa mashabiki wetu.
 
Cafonline.com: Ukiwa kama nahodha una ujumbe gani kwa wachezaji wenzio?
 
Hassan: Wachezaji wote wanajua wajibu wao na wanafikiria zaidi mchezo huu. Tuna imani tutapata ushindi ili kuwafurahisha wamisri wote.

Mechi nyingine hii leo ni GHANA v LESOHO itayochezwa mji wa Kumasi.











No comments:

Post a Comment