VIEW OTHER SITES

Monday

UHURU ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA


KIUNGO  Uhuru Suleiman Mwambungu ameongeza mkataba wake kwa miaka miwili na klabu yake, Simba SC na kufuta taarifa zilizomhusisha na Yanga waliokuwa wanamtaka mchezaji huyo.
Uhuru aliwasili Simba misimu miwili iliyopita akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, iliyomtoa Coastal Union ya Tanga amesema kwamba ameongeza mkataba wa miaka miwili na klabu yake.
“Kaka nimesaini mkataba mpya wa miaka miwili na hivi ninavyozungumza na wewe nimekuja kwetu Mbeya kijijini kabisa kuchukua baraka za wazee, kisha nirudi kazini na nguvu mpya,”alisema Uhuru.
Uhuru hakutaka kuwazungumzia Yanga, kwa sababu amesema hakuwahi hata kukaa nao meza moja zaidi ya kusikia tetesi kwamba wanamtaka.
“Nilisikia Yanga walikuwa wananitaka, ila kwa kweli mimi naona wamechelewa, kwa sababu nimekwishaongeza mkataba na timu yangu,”alisema.
Wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza Simba msimu huu, ambao mikataba yao imeisha ni mabeki Juma Nyosso na Juma Jabu, ambao nao wanahusishwa na mpango wa kuhamia kwa mahasimu wa jadi, Yanga. 

MANJI ATINGA JANGWANI KUCHUKUA FOMU


Mdhamini wa klabu ya soka ya Yanga, YUSSUF Mehboob Manji, ametinga makao makuu ya klabu hiyo na kuchukua fomu za kugombea nafasi ya uongozi klabuni humo, klabu hiyo iliyopo kwenye makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani leo mashabiki waliduwaa baada bosi huyo wa klabu ya Yanga kutinga kwenye ofisi za klabu hiyo hii leo.
Hata hivyo imetaarifiwa kuwa Manji amewachukulia fomu za kugombea uongozi, wanachama watatu, katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Julai 15, mwaka huu mjini Dar es Salaam mbali na yeye kuhusishwa na kutaka kugombea nafasi ya uenyekiti klabuni hapo.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili amesema kwamba Manji amewachukulia fomu wanachama watatu, ambao ni Abdallah Bin Kleb na Muhingo Rweyemamu kwa ajili ya nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji na Isaac Chanji kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Lakini bado kuna uvumi kwamba Manji mwenyewe wakati wowote atachukua fomu ya kuwania Uenyekiti, ingawa awali ilielezwa anamuunga mkono Francis Kifukwe awanie nafasi hiyo.
Kuchukua fomu kwa wajumbe hao watatu, kunafanya idadi ya waliochukua fomu hadi sasa kufika 10, baada ya awali Ayoub Nyenzi kuchukua fomu ya kugombea Makamu Mwenyekiti, Jumanne Mwamenywa, John Jambele, Peter Haule,
Gaudicius Ishengoma, Abdallah Sharia na Saleh Abdallah, wote Ujumbe.

KIEMBA, SHAMTE WAREJEA MSIMBAZI


Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Simba SC, Ibrahim Masoud ‘Maestro’ ametangaza kurejea kwa kiungo, Amiri Kiemba na Haruna Shamte leo mchana.
Kiemba aliyekataa kwenda kujiunga na Polisi Dodoma kwa kutokufikia makubaliano, wakati Shamte aliichezea Villa Squad iliyoshuka daraja.
Maestro akizungumza mchana huu amesema kwamba baada ya wachezaji hao kumaliza muda wao wa kuwa nje kwa mkopo, klabu itaangalia kama itawatoa tena kwa mkopo au itawarejesha kikosini.
Lakini habari za ndani zinadai kwamba wachezaji hao watarejeshwa kikosini, kwa sababu ya umuhimu wao na badala yake, beki Victor Costa na kiungo Salum Machaku ndio watatolewa kwa mkopo.  
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Simba SC, Ibrahim Masoud ‘Maestro’ amesema kwamba, Kiemba alikataa kabisa kwenda kuichezea Polisi Dodoma kwa sababu hawakufikia makubaliano, wakati Shamte aliichezea Villa Squad iliyoshuka daraja.
Baada ya wachezaji hao kumaliza muda wao wa kuwa nje kwa mkopo, klabu itaangalia kama itawatoa tena kwa mkopo au itawarejesha kikosini.

EPIQ BSS 2012 KUANZIA DODOMA


ZIARA ya kusaka vijana watakaoshiriki katika shindano la Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanza rasmi mkoani Dodoma Juni 15 katika Ukumbi wa Royal Village.

Akizungumzia ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Production Ritha Paulsen alisema kuwa washiriki wanatakiwa kufika katika ukumbi huo kuanzia saa 12 asubuhi.

Alisema kuwa kampuni yake inatarajia kuchukua vijana watatu hadi watano kutoka mkoa huo watakaouwakilisha mkoa huo katika fainali zitakazofanyikia Dar es salaam.

Alisema kuwa wakiwa mkoani humo wanatarajia kuona vipaji vya wasanii wa kila aina kwa kuwa EBSS inalenga kukuza vipaji vya vijana wenye uwezo wa kuimba aina zote za nyimbo.

“ Kama ambavyo imeshafahamika kuwa mwaka huu mshindi wa EBSS atapata kitita cha shilingi milioni 50 taslim hivyo ni kwamba tunawaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma wenye vipaji kuja kwa wingi siku hiyo” alisema Ritha

Ritha ataongozana na majaji wengine ambao ni Salama Jabir na Master Jay.

BAADHI YA WASHIRIKI WA BSS 2011 KUTOKA


 MKOANI ARUSHA WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA.

10 KALI UTATA VIWANJANI ..........

VIWANJA VITAVYOTUMIWA EURO 2012 NCHINI POLAND NA UKRAINE

FAINALI YA KWANZA YA MICHUANO YA ULAYA MWAKA 1960 KATI YA YUGOSLAVIA DHIDI YA USSR

SEHEMU YA MCHEZO KATI IVORY COAST DHIDI YA TANZANIA KUELEKEA BRAZIL 2014

KUYT ATUA RASMI FENERBAHCE BAADA YA MISIMU 6 AKIWA NA LIVERPOOL

MAGOLI NA ASSIST ZA SHINJI KAGAWA 2011/2012 AKIWA NA DORTMUND

BRAZIL HOI KWA MEXICO


Mabao mawili ya Javier Hernandez “Chicharito” na Giovani Dos Santos yameiwezesha Mexico kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Brazil kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Goli la kwanza la Mexico lilifungwa dakika ya 21 kupitia kwa Dos Santos kabla ya Chicharito kufunga goli la pili dakika ya 32 kwa njia ya mkwaju wa penati.
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Cowboys wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 84 519 ulikuwa wa kujipima nguvu kwa Brazil inayoshiriki mashindano ya Olimpiki mwezi Julai nchini Uingereza, huku Mexico ikijiandaa na mchezo wao na Guyana ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia nchini Brazil 2014.

NANI MKALI EURO 2012

Kikosi cha timu ya taifa ya Uhispania 
kilichotwaa kombe la Ulaya 2008
nchini Ujerumani.