VIEW OTHER SITES

Monday

WEBBER ATWAA UBINGWA MONACO GP

Dereva wa Red Bull, Mark Webber amefanikiwa kutwaa taji la mbio za magari za Monaco nchini Ufaransa kwa mara ya pili kwa kuwazidi Fernando Alonso wa Ferrari na Nico Rosberg wa Mercedes Benz.
Mbio hizo zenye umbali wa kilomita 3.340 sawa na maili 2.075 zilishuhudiwa kwa muaustralia, Webber akitwaa ubingwa wake wa pili wa Monaco GP akitumia muda wa 1:18.805.
WALIOINGIA KWENYE TANO BORA NA MUDA WALIOTUMIA
DEREVA                    TIMU             MUDA
1    Mark Webber         RED BULL         1:18.805
2    Nico Rosberg        MERCEDES BENZ    1:18.977
3    Fernando Alonso    FERRARI          1:18.857
4    Sebastian Vettel   RED BULL         1:19.076
5    Lewis Hamilton      McLAREN          1:18.806
Mbali na ushindi huo wa Webber katika viunga vya Monte Carlo na kutwaa taji kutoka kwa Vettel bingwa wa 2011 bado rekodi ilitowekwa na Michael Schumacher mwaka 2004 akitumia muda wa 1:14.439 ilishindwa kuvunjwa na Webber akizidiwa kwa sekunde 4.366.
Mwaka jana katika mbio za Monaco Webber alishika nafasi ya nne akitumia 1:16.234 nyuma ya Button, Alonso na Vettel.
Kwa ushindi huo Webber amejitwalia alama 25.

No comments:

Post a Comment