Klabu kongwe nchini Ghana ya Asante Kotoko imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2011/2012 nchini humo hii leo.
Timu hiyo imetwaa ubingwa huo baada ya kuifunga Tema Youth kwa goli moja bila majibu kupitia kwa Richard Yeboah iliyeunganisha krosi ya Kofi Nti_Boakye kutokea wingi ya kushoto dakika ya 57.
Mchezo huo uliopigwa kwenye mji wa Kumasi ulishudiwa na mashabiki lukuki wa Kotoko ambapo beki wa kushoto wa Kotoko, Gideon Baah alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo kutokana na kiwango alichokionesha kwa kuisumbua timu ya Tema Youth.
Kocha wa KOtoko, Maxwell Konadu alimjumuisha Ben Acheampong kwenye kikosi chake hii leo ambaye ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ghana “Black Stars” kitakachoikabili Lesotho mwishoni mwa wiki hii.
Nafasi ya pili imeenda kwa Ashanti Gold iliyofikisha alama 47 baada ya kuifunga Ebusua Dwarfs magoli 2-0 kwenye uwanja wa Sekondi kupitia kwa Mohamed Yakubu.
Matokeo mengine na miji ilikochezwa michezo hiyo,
Accra: Hearts 4-0 Arsenals
Dormaa: Aduana 1-0 Liberty
Wa: A. Stars 1-0 Medeama
Bekwai: New Edubiase 1-0 Bechem Utd
Berekum: Chelsea 1-1 Mighty Jets
MSIMAMO MZIMA BAADA YA KUMALIZA KWA LIGI HIYO HII LEO;
1 Asante Kotoko 30 18 9 3 42 18 24 59
2 AshantiGold FC 30 13 10 7 34 33 1 48
3 Adunana Stars 31 11 14 6 25 15 10 47
4 Hearts of Oak 30 13 10 7 31 19 12 46
5 Medeama SC 30 13 5 12 39 34 5 44
6 Liberty Professionals 30 11 9 10 38 29 9 42
7 Berekum Chelsea 30 11 12 7 30 23 7 41
8 Edubiase FC 30 13 5 12 34 36 -2 38
9 Tema Youth 30 9 9 12 31 30 1 35
10 WA All Stars 30 10 10 10 19 20 -1 34
11 Dwarfs 30 9 10 11 23 25 -2 33
12 Arsenals 31 7 10 14 24 40 -16 31
13 Heart of Lions 30 7 11 12 21 31 -10 29
14 Wassaman United 30 7 8 15 27 42 -15 29
15 Mighty Jets 30 5 14 11 23 29 -6 28
16 Bechem United 30 5 12 13 24 41 -17 27
No comments:
Post a Comment