Kocha wa klabu ya Juventus mabingwa wa Serie A ameingia matatani kwa tuhuma za kuhusika na upangaji wa matokeo nchini humo.
Tukio hilo limepelekea kukamatwa kwa nahodha wa klabu ya Lazio, Stefano Mauri mwenye miaka 32 kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tukio hilo akiwa pamoja na nahodha mstaafu na kiungo wa Genoa, Omar Milanetto.
Maafisa wa polisi walienda kwenye kambi ya timu yataifa ya Italia ili kufanya mahojiano na beki wa kushoto wa Italia na klabu ya Zenit St. Petersburg ya Urusi, Domenico Criscito mwenye miaka 25.
Hata polisi nchini humo bado inatafuta makazi 30 ya wachezaji, wakufunzi na viongozi wa vilabu vinavyoshiriki ligi za nchini huma ikiwemo Serie A, Serie B na madaraja ya chini.
Polisi imesema Conte anashikiliwa kutokana na kuhusishwa na upangaji matokeo akiwa na klabu yake ya zamani Siena wakati ikicheza na Novara Aprili,2011, hata hivyo wakili wa Conte, Antonio De Rencis, amesisitiza kuwa mteja wake hausiki na tukio lolote la upangaji matokeo nchini humo.
Naye makamu wa rais wa shirikisho la soka nchini humo, Demetrio Albertini ametangaza kuwa Cristico ambaye ni beki wa zamani wa Genoa na Juventus hatochaguliwa kwenye kikosi kitakachoshiriki michuano ya Ulaya nchini Ukraine na Poland hadi atakapoonekana hana hatia.
Wengine waliokumbwa na mkasa huo ni Leonard Bonucci beki wa Juventus alipokuwa na klabu ya Bari.
No comments:
Post a Comment