VIEW OTHER SITES

Monday

UHURU ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA


KIUNGO  Uhuru Suleiman Mwambungu ameongeza mkataba wake kwa miaka miwili na klabu yake, Simba SC na kufuta taarifa zilizomhusisha na Yanga waliokuwa wanamtaka mchezaji huyo.
Uhuru aliwasili Simba misimu miwili iliyopita akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, iliyomtoa Coastal Union ya Tanga amesema kwamba ameongeza mkataba wa miaka miwili na klabu yake.
“Kaka nimesaini mkataba mpya wa miaka miwili na hivi ninavyozungumza na wewe nimekuja kwetu Mbeya kijijini kabisa kuchukua baraka za wazee, kisha nirudi kazini na nguvu mpya,”alisema Uhuru.
Uhuru hakutaka kuwazungumzia Yanga, kwa sababu amesema hakuwahi hata kukaa nao meza moja zaidi ya kusikia tetesi kwamba wanamtaka.
“Nilisikia Yanga walikuwa wananitaka, ila kwa kweli mimi naona wamechelewa, kwa sababu nimekwishaongeza mkataba na timu yangu,”alisema.
Wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza Simba msimu huu, ambao mikataba yao imeisha ni mabeki Juma Nyosso na Juma Jabu, ambao nao wanahusishwa na mpango wa kuhamia kwa mahasimu wa jadi, Yanga. 

No comments:

Post a Comment