VIEW OTHER SITES

Thursday

VILLAREAL YAPOTEZA KOCHA NDANI YA SAA 24


Imebadilishwa:
Kocha wa klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho ameongoza maelfu ya watu katika kutoa heshima zao kwa aliyekuwa kocha mpya aliyeteuliwa na klabu ya Villareal, Manuel Preciado ambaye amefariki saa 24 baada ya kutangazwa kuiongoza klabu hiyo nchini Uhispania.
Precado alikuwa kocha wa Sporting Gijon klabu ya mkataba huo alifariki kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 54 huko jijini Valencia.
Kifo chake kimetokea saa 24 baada ya kusaini mkataba wa kuiongoza klabu ya Villareal iliyoshuka daraja, ambapo mkataba wake ulitarajiwa kuanza rasmi msimu wa mwaka 2012 hadi 2013.
Preciado alifukuzwa kazi na Sporting Gijon mnamo mwezi Januari licha ya kuiwezesha klabu hio kupanda daraja mara mbili kuingia Ligi kuu ya Uhispania, La Liga na kuifundisha kwenye mechi 232 kama kocha mkuu akiwa miongoni mwa makocha walioifundisha klabu hiyo kwa mafanikio zaidi nyuma ya Jose Manuel Diaz Novoa aliyeifundisha klabu kwenye mechi 282.
Enzi za uchezaji wake Preciado alicheza kama beki akianzia klabu ya Racing Santander kisha vilabu kama Linares, Mallorca, Alaves, Ourense na Gimnastica.
Mwaka 1992baada ya kustaafu soka aliaanza shughuli za ukufunzi akianzia klabu ya Gimnastica baadaye Racing B, Racing Santander, Levante na Murcia kabla ya kujiunga na Sporting Gijon mwaka 2006.

No comments:

Post a Comment