Mdhamini wa klabu ya
soka ya Yanga, YUSSUF Mehboob Manji, ametinga makao makuu ya klabu hiyo na
kuchukua fomu za kugombea nafasi ya uongozi klabuni humo, klabu hiyo iliyopo kwenye
makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani leo mashabiki waliduwaa baada bosi huyo
wa klabu ya Yanga kutinga kwenye ofisi za klabu hiyo hii leo.
Hata hivyo
imetaarifiwa kuwa Manji amewachukulia fomu za kugombea uongozi, wanachama
watatu, katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Julai 15, mwaka huu mjini Dar es
Salaam mbali na yeye kuhusishwa na kutaka kugombea nafasi ya uenyekiti klabuni
hapo.
Katibu Mkuu wa
Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili amesema kwamba Manji
amewachukulia fomu wanachama watatu, ambao ni Abdallah Bin Kleb na Muhingo
Rweyemamu kwa ajili ya nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji na Isaac Chanji
kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Lakini bado kuna uvumi
kwamba Manji mwenyewe wakati wowote atachukua fomu ya kuwania Uenyekiti, ingawa
awali ilielezwa anamuunga mkono Francis Kifukwe awanie nafasi hiyo.
Kuchukua fomu kwa
wajumbe hao watatu, kunafanya idadi ya waliochukua fomu hadi sasa kufika 10,
baada ya awali Ayoub Nyenzi kuchukua fomu ya kugombea Makamu Mwenyekiti,
Jumanne Mwamenywa, John Jambele, Peter Haule,
Gaudicius Ishengoma,
Abdallah Sharia na Saleh Abdallah, wote Ujumbe.

No comments:
Post a Comment