ZIARA ya kusaka vijana
watakaoshiriki katika shindano la Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanza
rasmi mkoani Dodoma Juni 15 katika Ukumbi wa Royal Village.
Akizungumzia ziara hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Production Ritha Paulsen alisema
kuwa washiriki wanatakiwa kufika katika ukumbi huo kuanzia saa 12 asubuhi.
Alisema kuwa kampuni yake
inatarajia kuchukua vijana watatu hadi watano kutoka mkoa huo watakaouwakilisha
mkoa huo katika fainali zitakazofanyikia Dar es salaam.
Alisema kuwa wakiwa
mkoani humo wanatarajia kuona vipaji vya wasanii wa kila aina kwa kuwa EBSS
inalenga kukuza vipaji vya vijana wenye uwezo wa kuimba aina zote za nyimbo.
“ Kama ambavyo
imeshafahamika kuwa mwaka huu mshindi wa EBSS atapata kitita cha shilingi
milioni 50 taslim hivyo ni kwamba tunawaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma wenye
vipaji kuja kwa wingi siku hiyo” alisema Ritha
Ritha ataongozana na majaji wengine ambao ni Salama Jabir na Master
Jay.
![]() | |||||
| BAADHI YA WASHIRIKI WA BSS 2011 KUTOKA |


No comments:
Post a Comment