VIEW OTHER SITES

Sunday

CZECH, UGIRIKI ZAWASILI POLAND

Timu za taifa za Czech na Ugiriki zimekuwa za kwanza kufika nchini Poland kwa michuano ya Ulaya 2012 huku ikiwa zimebakia siku tano kabla ya kunza kwa michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.
Timu zote zimepangwa kundi moja la A pamoja na Poland na Urusi, ambapo mechi za kwanza zinatarajiwa kuchezwa ijumaa wiki hii kwa Poland kufungua dimba na bingwa wa 2004,Ugiriki kwenye mji mkuu Warsaw huku Urusi akicheza na Jamhuri ya Czech kusini magharibi mwa mji wa Wroclaw.
Jamhuri ya Czech imewasili Wroclaw kutokea Prague kwa usafiri wa garimoshi lenye rangi nyekundu, nyeupe na bluu zinazovaliwa na timu hiyo zikiwemo kwenye bendera ya taifa lao, huku Ugiriki wakiwasili kwenye mji wa Warsaw.
Czech wataingia uwanja wakiwa na nahodha wao, Thomas Roscicky aliyepata majeraha madogo ambapo madaktari wa timu wamethibitisha kuwa atashiriki kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Urusi huku akitarajiwa kukutana na nahodha wa Urusi na mchezaji mwenzake wa zamani wa   Arsenal, Andrey Arshavin.
Hata hali ya usalama inaelekea kutiwa doa nchini humo kufuatia mpango wa kufanya maandamano ulioandaliwa na kikundi cha watu wanaoipinga serikali mpya ya Bronislaw Komorowski waliopanga kuandamana Juni, 10.


No comments:

Post a Comment