Klabu
ya soka ya Liverpool maarufu kama majogoo wa jiji imeamua kumwachilia mshambuliaji wake raia wa Uholanzi,
Dirk Kuyt(pichani) mwenye miaka 31 baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu 6 akitokea
Feyernoord ya Uholanzi.
Kuyt
anatarajiwa kujiunga na Fernabahce ya Uturuki siku chache zijazo kulingana na taarifa za mtandao wa klabu ya
Liverpool, ambao hivi karibuni imemsajili kocha mpya, Brendan Rogders kutoka
Swansea City.
Kuyt
ambae anajiandaa na michuano ya Ulaya inayofanyika nchini Poland na Ukraine
alijiunga na Liverpool 2006 akitokea Feyernoord ya Uholanzi akicheza mechi 285
na magoli 71 ikiwemo matatu (hat trick) dhidi ya Manchester United msimu
ulipita.
Kuyt
pia alifunga goli mojawapo kwenye mchezo wa fainali ya kombe la ligi mwezi
Februari dhidi ya Cardiff City kwenye uwanja wa Wembley.

No comments:
Post a Comment