VIEW OTHER SITES

Saturday

MANJI KUANZA KAZI RASMI KESHO

Hapo kesho majira ya saa 4:00 asubuhi, uongozi mpya wa klabu ya soka ya  Yanga utaingia rasmi kwa kuapishwa na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini, Mama Fatuma Karume kwenye makao makuu ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam.
Kisha wachezaji na viongozi wa Yanga wataelekea mkoani Dodoma kufuatia mwaliko wa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wapenzi wa klabu hiyo siku ya Jumatatu.
Mwaliko huo unatokana na kulitwaa taji la klabu bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati,Kagame, Jumamosi iliyopita, wakiifunga Azam FC mabao 2-0 kwenye fainali, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Julai 15, mwaka huu, Yanga ilipata uongozi mpya chini ya uenyekiti wa, Yussuf Manji, Makamu wake akiwa, Clement Sanga na wajumbe wanne wa kamati ya utendaji, Abdallah Bin Kleb, George Manyama na Mussa Katabaro.
Wajumbe wengine waliosalia kutoka uongozi uliopita, Mohamed Bhinda, Titto Osoro, Salim Rupia na Sarah Ramadhan baada ya wajumbe wengine, wakiwemo Mwenyekiti, Wakili Lloyd Nchunga na Makamu wake, Davis Mosha kujiuzulu.   

No comments:

Post a Comment