VIEW OTHER SITES

Friday

ROLLINGSTON YAFIKIA UKINGONI


Timu ya Coastal Union ya chini ya miaka 17 itamenyana na Ecofoot ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),kwenye mchezo wa fainali ya mashindano ya Rollingston hapo kesho.

Coastal imetinga hatua hiyo baada ya kuwafunga mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Ruvu Shooting kwa mabao 2-1 nchini Burundi.

Mabao ya Coastal yakiwekwa kimiani na Mohamed Miraji, wakati bao la Ruvu likifungwa naye, Said Hussein.

Timu ya Ecofoot imetinga hatua kufuatia ushindi wao dhidi ya Mjini Magharibi ya Zanzibar wa mabao 2-1.

Mabao ya Ecofoot yalitiwa kimiani na Sais Kabamba na Shukuru Hamisi, wakati bao la kufutia machozi la Mjini Magharibi lilitiwa kimiani na Omar Tamim. Sasa, Mjini Magharibi itamenyana na Ruvu katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu na Coastal itamenyana na Ecofoot katika mechi ya kusaka bingwa mpya wa michuano hiyo kesho. 

No comments:

Post a Comment