Kocha wa Konkola Mine Police, Masauso Mwale anachukua nafasi ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanawake akisaidiwa na Enala
Simbeye Phiri na Kaluba Kangwa.
Wengine ni Besa Chibwe meneja wwa timu, Dorothy Mabomahoko na Cornelia Chazura wanakuwa daktari na mtaalamu wa mifupa.
Timu ya taifa ya wanawake ya chini ya miaka 17 kocha mkuu kuwa,
Albert Kachinga akisaidiwa na Masiye
Mukwasa na Kape Saili. Meneja wa timu kuwa, Clementina Mazuba, wakati Womba
Kadochi anakuwa daktari wa timu na Chabu Bwalya kuwa mtaalamu wa mifupa.
Timu ya chini ya miaka 20, kocha mkuu kuwa, Chris Kaunda lakini kabla Kaunda alikuwa kocha mkuu wa timu ya chini ya miaka 17 na sasa atafanya kazi na kocha wa sasa wa Zanaco, Keegan Mumba na kocha msaidizi wa Power Dynamos, Hector
Chilombo.
Lighton Ndashe wa Lime Hotspurs ameteuliwa kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya wanaume cha chini ya miaka 20 cha Zambia akichukua nafasi ya Stanley Kaseko ambaye anachukua nafasi nyingine kwenye timu ya taifa ya wakubwa "Chipolopolo" wakati Daktari George Magwende na Peter Phiri wanaendelea kuwa matabibu wa timu hiyu.
Nayo timu ya U17 ya wanaume itakuwa na kocha msaidizi wa Green Buffaloes’ Bilton
Musonda hkama kocha msaidizi wa U17 wanaume. Osward Mutapa anabakia kama kocha mkuu huku kocha wa zamani wa Nkana, Linos Makwaza akiwa msaidizi wake. Daniel
Jere atabakia kama meneja wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment