VIEW OTHER SITES

Saturday

KENYA U17: 20 WATEULIWA NA FKF





SHIRIKISHO la SOka nchini Kenya (FKF) limeteua wachezaji 20 watakaounda kikosi cha timu ya taifa U17 kitakachoikabili Tanzania ili kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17.
Wachezaji hao hao wanatarajiwa kufanyiwa vipimo vya MRI ili kutambua miaka yao sahihi likiwa ni agizo la shirikisho la soka barani afrika (CAF).
Wachezaji hao wanatokana na michuano ya Copa Coca Cola na mashindano ya vijana nchini humo.
Kwa upande mingine FKF imeandaa mechi za kirafiki kwa timu dhidi ya timu za majimbo, mataifa mengine pamoja na klabu za ligi kuu nchini humo kabla kuingia kambini Agosti 20 kwa ajili ya mafunzo.
Timu hiyo iko chini ya Kocha mkuu David Ouma na wasaidizi wake, Eliud Omukuiya na Kinero Swaleh, huku Jabir Hassan akiwa mkufunzi wa makipa na meneja wa timu ni Sammy Okoth.
Kikosi kamili kinaundwa na Omar Musa, Isaack Aliwa, Eugine Moses, Stephen Ogweno, Apolo Otieno, James Mazembe, Sylvester Godwin, Ibrahim Moge, Alfred Wekesa, Eugine Chege, Castro Mwaura, Robert Mutua, Boniface Mwenda, Kelvin Otieno, Peter Mwaguna,Shaubi Rashid, William Waithaka, Oruchum Christopher, Edwin Mukolwe, Moses Mwangi.

No comments:

Post a Comment