VIEW OTHER SITES

Saturday

RED BULL YAMSIKILIZIA OKWI

Klabu ya FC Red Bull Salzburg ya nchini Austria wenda ikasitisha mpango wake wa kumsajili mshambuliaji wa Simba SC na timu ya taifa ya Uganda, Emmanuel Arnold Okwi, licha kufuzu majaribio katika klabu hiyo kwa wiki tatu alizokuwa nchini humo akifanyiwa majaribio.
Habari kutoka Simba SC zimesema kuwa, Okwi amekwama na anarejea Simba SC, huku kukiwa na uvumi unaomhusisha mshambuliaji huyo wa zamani wa SC Villa ya Uganda na kuelekea mtaa wa Jangwani ikiwa ni mipango ya uongozi mpya wa Yanga kuimarisha safu ya ushambuliaji.
Kwa sasa Okwi yuko nchini Uganda kutoka Austria, kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa Malaria.
Hata hivyo Katibu wa Simba Evodius Mtawala amesema kuwa; “Okwi amefuzu majaribio, ila ana Malaria, amekuja kuitibu kisha atarudi Austria kwa ajili ya vipimo,”alisema Mtawala.
Klabu hiyo ya Austria ilipanga kuipa Simba SC Euro 600,000,
Hapo kabla, Simba ilipata ofa ya Sh. Bilioni 2 kutoka kwa miamba ya soka ya Afrika Kusini, Mamelodi Sundown lakini mshambuliaji huyo hakuwa tayari kujiunga na klabu hiyo.
Lakini pia, Olando Pirates ya Afrika Kusini ilimuomba Okwi akafanye majaribio huko kama angefuzu wangemsajili dau la dola 550,000 kabla ya kuibuka kwa taarifa za kutakiwa na klabu ya Parma ya Italia.

No comments:

Post a Comment