Schlupp, 20, ambaye hucheza nafasi ya ushambuliaji amekuwa kwenye mazoezi uwanja wa Carrington akiwa na ruhusa kutoka kwenye klabu yake, ambayo imekuwa na mahusiano ya karibu na United na mara kadhaa imekuwa ikichukua wachezaji kwa mkopo kutoka Manchester United.
Schlupp si mchezaji mwenye uzoefu hata kwenye ligi daraja la kwanza kwani mara ya mwisho kuchezea kikosi cha kwanza ilikuwa mwezi Novemba mwaka jana. Miongoni mwa vitu vilivyoivutia klabu hiyo ni uwezo wake wa kucheza kama mshambuliaji wa pembeni lakini pia kama beki wa kushoto kwenye klabu yake.
Zao hilo la kituo cha kukuza vipaji cha Leicester City kabla ya kuibuka msimu uliopita kwenye kikosi cha kwanza pia alicheza kwa mkopo klabu ya Brentford 2010-2011, huku akiifungia klabu yake mabao matatu (hat-trick) katika mchezo wake wa kwanza wa ligi daraja la kwanza akiwa na Leicetser dhidi ya Rotherham United katika kombe la ligi.
Mbali na kuwa uraia wa Ghana lakini ametumikia kikosi cha vijana cha Ujerumani, akiwa mzaliwa wa Hamburg kabla ya kuelekea nchini Uingereza akiwa bado mdogo kwa sasa ana mkataba na klabu yake unaombakisha hadi 2015.
| Date of birth | 23 December 1992 | ||
|---|---|---|---|
| Place of birth | Hamburg, Germany | ||
| Height | 1.81 m (5 ft 11 1⁄2 in) | ||
| Playing position | Forward / Left winger / Left back | ||
| Club information | |||
| Current club | Leicester City | ||
| Number | 18 | ||
| Youth career | |||
| 2005–2010 | Leicester City | ||
| Senior career* | |||
| Years | Team | Apps† | (Gls)† |
| 2010– | Leicester City | 27 | (2) |
| 2011 | → Brentford (loan) | 9 | (6) |
| National team‡ | |||
| 2010 | Germany U19 | ||
| 2011 | Ghana | 1 | (0) |

No comments:
Post a Comment