VIEW OTHER SITES

Friday

MWISHO WA KUCHUKUA FOMU TFF LEO




Wakati zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) likitarajiwa kumalizika hii leo waombaji 36 wameshachukua huku 18 wakiwa wamesharejesha fomu hizo.

Idadi hiyo ni kufikia jana mchana (Januari 17 mwaka huu). Pia Kamati ya Uchaguzi ya TFF imesisitiza kuwa wanaorejesha fomu hizo kwa barua pepe wanatakiwa kuzituma kwa Katibu Mkuu wa TFF kupitia tfftz@yahoo.com na si kwa email binafsi za wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi au maofisa wa TFF.

Waombaji wanne walioongezeka katika orodha ni Blassy Kiondo kwa Kanda ya Katavi na Rukwa, Eliud Mvella (Mbeya na Iringa), Geofrey Nyange (Morogoro na Pwani), na Omari Abdulkadir kwa Kanda ya Dar es Salaam.

Orodha kamili ya waombaji ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais) wakati waombaji wa umakamu wa rais mpaka sasa ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia.

Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).

Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).

Athuman Kambi na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Nyange na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala na Eliud Mvella (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).

Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf Manji amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti.

No comments:

Post a Comment