VIEW OTHER SITES

Friday

KIPLAGAT: SSMB HAIKUPEWA 350 MILIONI NA SERIKALI

Mwenyekiti wa chama cha riadha nchini Kenya (AK), Isaiah Kiplagat amemtaka waziri wa michezo nchini humo, Ababu Namwamba kufuatilia kwa umakini kauli yake kufuatia kauli ya waziri huyo kuwa serikali ya Kenya imetoa shilingi milioni 350 kwa bodi ya usimamizi wa viwanja vya michezo (SSMB).

Kiplagat ambaye ni mjumbe wa bodi hiyo amesema kuwa bodi yake imepatiwa shilingi milioni 70 kwa ajili ya ukarabati wa Kipchoge uliopo Eldoret kutoka kwenye milioni 100 ambazo zilitengwa kwa ajili ya vifaa vya michezo.

Kauli ya waziri huyo imeleta mkanganyiko na bodi hiyo kutokana na ukweli kuwa fedha hizo zilikabidhiwa kwa kitengo cha michezo kinachojihusisha na maendeleo ya miundombinu ya michezo chini ya wizara hiyo na si bodi hiyo.

Kiplagat amesema kuwa waziri wa michezo, Namwamba ameshauriwa vibaya kuhusu zilikopelekwa fedha hizo, na kwamba bodi hiyo imepokea fedha za ukarabati wa viwanja na kuendesha taasisi hiyo tu.

Wawili hao wanadaiwa kukwaruzana wakati wa ufunguzi wa shule ya kukuza vipaji ya Lornah Kiplagat iliyopo Iten, huku Kiplagat akidai kuwa hana mawazo mabaya dhidi ya waziri huyo.

"Waziri hajashauriwa vizuri kuhusu kazi za SSMB na ndio maana alizungumza kitu ambacho hakifahamu," alisema.

Aliongeza kuwa, kwa kaulia ya waziri inamaanisha SSMB haikuumia vizuri fedha hizo kitu ambacho si kweli, na kwamba waziri huyo alitakiwa kupewa taarifa sahihi kuhusu uhusiano uliopo baina ya wizara na bodi hiyo.

Kiplagat alimalizia kwa kusema kuwa hausiki na upotevu wa msaada kamati ya olimpiki ya 2004 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja North Rift, lakini pia akimtaka waziri huyo kutatua matatizo kwa njia ya amani na mazungumzo na si kutumia vitisho

No comments:

Post a Comment