SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) linampongeza Amani Ibrahim Makungu kwa kuchaguliwa kuwa
Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) katika uchaguzi uliofanyika
juzi (Juni 30 mwaka huu) kwenye hoteli ya Bwawani, mjini Zanzibar.
Ushindi
wa asilimia 94 alioupata Makungu ambaye hakuwa na mpinzani katika uchaguzi huo
mdogo unaonesha imani ambayo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA wanayo kwake katika
kukiongoza chama hicho.
Ni
matarajio ya TFF kuwa ushindi huo utatafsiriwa kwa vitendo na wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa ZFA na wadau wa mpira wa miguu Zanzibar kwa kumpa Makungu
ushirikiano wa asilimia 100 ili kuhakikisha Kamati yake ya utendaji inafanya
kile kinachotarajiwa na wengi.
Makungu
si mgeni katika mpira wa miguu, na mchango aliotoa kwa mchezo huo visiwani
kabla ya kuwania nafasi hiyo unatambuliwa na kila anayefuatilia maendeleo ya
mpira wa miguu katika Zanzibar.
TFF
tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa ZFA chini ya Makungu kama ilivyokuwa
kwa mtangulizi wake Ali Ferej Tamim ili kuhakikisha ustawi wa mpira wa miguu
visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Makungu pia amepata kuwa mfadhili wa klabu ya Miembeni ya visiwani humo.

No comments:
Post a Comment