Kocha
wa zamani wa Taifa Stars, Mbrazili Marcio Maximo amewasili nchini ili kumalizia
mazungumzo yao ya kuingia mkataba na klabu ya Young Africans “Yanga”
kuifundisha kwa msimu ujao.
Yanga
ambao wameamua kukutana na kocha huyo baada ya kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa
klabu hiyo, Mserbia Konstadin Papic ambaye aliondoka mwishoni mwa msimu
uliopita kuelekea kwao.
Maximo
alikuwa na Stars kutoka 2006 hadi 2010 mkataba wake ulipomalizika kabla ya
Mdenimaki Jan Poulsen kuchukua nafasi yake.
Mwaka
2009 aliiwezesha Tanzania kushiriki mashindano ya afrika wa wachezaji wa ndani
yaliyofanyika nchini Ivory Coast.
Yanga
ambayo inatarajiwa kufanya uchaguzi wake mnamo Juni 17 imemaliza nafasi ya 3
kwenye ligi kuu ya Vodadom msimu huu, inatarajiwa kushiriki mashindano ya
Afrika Mashariki na Kati baadaye mwaka huu pekee kwenye medani ya kimataifa
ikiingia kama bingwa mtetezi.

No comments:
Post a Comment