Beki
wa zamani wa Argentina, Gabriel Alejandro Milito ametangaza kustaafu soka
mwishoni mwa msimu huu baada ya kudumu kwa miaka 15 akiwa na vilabu tofauti barani Amerika ya
Kusini na Ulaya.
Milito
mwenye miaka 31 ambaye pia ni ndugu wa Mshambuliaji wa Inter Milan, Diego
Milito amechezea vilabu mbalimbali ikiwemo FC Barcelona, Real Zaragoza na sasa akiwa
na Independiente kama nahodha wa klabu hiyo.
Milito
ameanza soka lake na Independiente akiwa na mika 17 mwishoni mwa mwaka 1997
hadi 2003 alipohamia Zaragoza ya Uhispania akicheza kwa misimu minne ya
mafanikio kabla hajasaini na Barcelona 2007 ambapo aliachana nayo mwaka 2011.
Amepata
kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina kwenye michezo 42 ikiwemo kombe la
dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani.
Milito amezaliwa Septemba 7, 1980 jijini Bernal, Argentina.
MATAJI ALIYOTWAA;
Independiente
Argentine League: (1) Apertura 2002
Zaragoza
Kombe la Uhispania: (1) 2004
Barcelona
Ligi ya Uhispania(3): 2009, 2010, 2011
Kombe la Uhispania (1): 2009
Klabu bingwa Ulaya(2): 2009, 2011
Argentine League: (1) Apertura 2002
Zaragoza
Kombe la Uhispania: (1) 2004
Barcelona
Ligi ya Uhispania(3): 2009, 2010, 2011
Kombe la Uhispania (1): 2009
Klabu bingwa Ulaya(2): 2009, 2011
No comments:
Post a Comment