VIEW OTHER SITES

Wednesday

BAUP KUMRITHI DESCHAMPS MARSEILLE


Klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa imemtangaza kocha mpya wa klabu hiyo baada ya kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Didier Deschamps hapo jana.
Kocha huyo, Elie Baup ametangazwa rasmi huku akisaini mkataba wa miaka miwili na miamba hiyo ya Ufaransa ambayo msimu uliopita ilimaliza nafasi ya 10 ya msimamo wa ligi kuu nchini humo.
Baup mwenye miaka 57 amejiunga na Marseille akitokea Girondins Bordeaux ambayo msimu wa 1999 aliisaidia kutwaa ubingwa wa Ufaransa lakini pia akiifundisha timu ya Aquitaine kuanzia 1998 hadi 2003.
Vilabu vingine amezifundisha St. Etiene, Toulouse na Nantes kwenye ligi ya nchini humo daraja la pili na amepata kuwa mchambuzi wa michezo kwenye vituo vya runinga nchini Ufaransa kwa miaka 3.
Deschamps ameondoka klabuni hapo jumatatu akiwa amebakiwa na mwaka mmoja kwenye mkataba wake.

No comments:

Post a Comment