VIEW OTHER SITES

Saturday

MISS UTALII TANZANIA YAGAWANYWA KIKANDA


Bodi ya Taifa ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania imegawa mikoa yote ya Tanzania na Vyuo Vikuu katika kanda maalumu za mashindano hayo.
  Kuanzia mwaka huu kutakuwa na kanda 14, zikiwemo saba (7) za kawaida na saba (7) kanda maalumu za Miss Utalii vyuo Vikuu.  
Hatua hiyo imelenga kufikisha mashindano hayo katika ngazi za chini zaidi ambapo kwa kuanzia mashindano haya yataanzia katika ngazi za kata, majimbo ,wilaya,mikoa, kanda, taifa na hatimaye dunia, huku mpango mkakati ni kuanza kufanyika katika mgazi za vijiji ifikapo mwaka 2014. 
 Mgawanyo wa kanda hizo na mikoa yake katika mabano ni:

A: KANDA ZA KAWAIDA NI:
1. Miss Utalii Tanzania –Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara, Zanzibar)
2. Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Magharibi (Simiyu, Shinyanga na Mara)
3. Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Ziwa (Mwanza, Geita, Kagera na Kigoma)
4. Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kaskazini (Arusha, Kilimanjaro na Arusha)
5. Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kati (Tabora, Dodoma, Singida na Morogoro)
6. Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kusini Nyanda za Juu (Mbeya, Rukwa na Katavi)
7. Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kusini (Ruvuma, Iringa na Njombe)

B: KANDA MAALUM ZA VYUO VIKUU NI:
1. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kati (Dodoma, Kigoma, Tabora, Singida)
2. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kusini (Iringa, Ruvuma, Njombe)
3. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Pwani (Dar es Salaam, Zanzibar , Lindi na Mtwara)
4. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu- Kanda ya Magharibi (Mwanza, Geita, Kagera, Mara, Simiyu, Shinyanga na Singida)
5. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kusini Nyanda za Juu (Mbeya, Rukwa, Katavi)
6. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kaskazini ( Arusha,Kilimanjaro,Manyara)
7. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Mashariki (Morogoro, Mtwara na Lindi)

Mgawanyo huu wa kanda umezingatia , maeneo ya kijografia, mwingiliano wa tamaduni, uwepo wa vivutio vya Utalii katika kila kanda, urahisi wa kutangaza Utalii na kuhamasisha Utalii wa ndani,pia kutoa fulsa kwa mabinti wengi zaidi kushiriki mashindano haya katika Ngazi zote.

Kwa mwaka huu, kanda ya ziwa ndiyo itakayo kuwa ya kwanza kufanya Fainali zake za Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012 na kushirikisha jumla ya warembo 15 kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Geita na Kigoma. 

Shindano hilo limepangwa kufanyika Juni 30, 2012 katika ukumbi wa Monarch Hotel Mwanza.

No comments:

Post a Comment