Klabu ya soka ya YANGA
imefanikiwa kumbakisha mshambuliaji wake, Jerryson Tegete ambaye amesaini
mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga hadi 2014.
Jerry amesema
kwamba amesaini mkataba wa miaka miwili zaidi kuendelea kuichezea Yanga. “Nimesaini leo, mimi ni mchezaji halali wa Yanga, kweli kabla ya kusaini na
hali ya mambo ilivyokuwa Yanga niliwahi kufanya mazungumzo na
viongozi wa Simba na Azam, ilikuwa tunaelekea kukubaliana, ila sasa
nashukuru hali imetulia klabuni, nami nimesaini leo,”alisema Tegete.
Habari zisizo na shaka
kutoka mitaa ya Twiga na Jangwani zinasema kwamba Tegete ambaye amemaliza
mkataba wake mwezi huu, amesaini kwa watu ambao wamepewa kazi ya kufanya zoezi
la usajili, Abdallah Ahmad Bin Kleb na Seif Ahmad ‘Magari’.
Simba imeshindwa
kuwabakisha kipa wao, Ally Mustafa Mtinge ‘Barthez’ na beki wa kati Kelvin
Patrick Yondan “Vidic” ambao wamekubali kusaini Yanga.
Jerry alitua Yanga
mwaka 2008, akitokea sekondari ya Makongo na kujihakikishia namba kwenye timu
hiyo kwa kupachika mabao hususani katika mechi zilizowakutanisha watani wa jadi.
Kwa upande wao Simba wamemsajili Kigi Makasi kutoka kwa mahasimu wao.

No comments:
Post a Comment