VIEW OTHER SITES

Saturday

UMISSETA MWANZA YAFUNGWA JANA

Mashindano ya UMMISETA jijini Mwanza yamemalizika hapo jana kwenye viwanja vya shule ya sekondari Nsumba huku wilaya za Geita na Misungwi zikishiriki kwa mara ya mwisho kama wilaya za mkoa Mwanza.

Mashindano hayo ambayo yalishirikisha shule za sekondari pekee kutoka wilaya za Mwanza kama Geita, Magu, Kwimba, Sengerema, Misungwi, Nyamagana, Ilemela na Ukerewe ambapo pia yalishuhudiwa kwa uteuzi wa timu za mkoa kwa upande wa soka, kikapu, pete, riadha, wavu, bao, mikono na tenisi ya mezani.

Mabingwa wa mashindano hayo wakiwa kwenye mabano na michezo yao ni Nyamagana (soka wasichana), Kwimba (soka wavulana), Sengerema (kikapu wavulana), Nyamagana (Kikapu wasichana), Sengerema (Geita), Ukerewe (mikono wavulana), Geita (mikono wasichana), Kwimba (wavu wasichana), Nyamagana (wavu wasichana), Geita (riadha wavulana na wasichana), Nyamagana (tenisi -mezani) na Misungwi (bao).

Lakini kulikuwa na uteuzi wa viongozi wa timu ya mkoa wakiongozwa na Mwalimu Kivagae, daktari Patrick Luzagi kwa upamde wa nyota waliong'ara kwenye mashindano hayo ni Hamida Athumani (Soka wasichana) aliyefunga magoli 7, Mabura Cloud (Soka wavulana) magoli 3, Saba Pastory (Kikapu), Mathayo Mathias (Bao), Elias John (Tenisi Mezani), Mussa Venance (Mikono wavulana ) na Salome Ademba (wasichana), Baraka Nyagawa (Riadha wavulana) na Metilda Paul (wasichana) Bathlomeo Revocatus (Wavu wavulana) na Rose Martin (wasichana).

Zawadi za jumla zilienda kwa Misungwi (Usafi na Nidhamu) na mshindi wa jumla wa mashindano akiwa wilaya ya Sengerema. Timu hiyo ya mkoa itaenda mkoani Mara baadaye Juni 17 kwa ajili ya mashindano ya kanda ya ziwa yenye mikoa ya Mwanza na Mara.

No comments:

Post a Comment