VIEW OTHER SITES

Saturday

Ghana yaiua Lesotho kuelekea Brazil 2014


Timu ya taifa ya Misri hapo jana ilifanikiwa kupata ushindi wa 2 -0 dhidi ya Msumbiji kwenye mchezo wa kufuzu ili kushiriki kombe la dunia 2014 nchini Brazil kwenye uwanja wa jeshi jijini Alexandria.
Ushindi kama huo iliupata mwaka 1990 dhidi ya Msumbiji, huku mlinzi Mahmoud Fathallah alifunga goli la kwanza kabla ya mlinda mlango Joao Kampango akijifunga mwenyewe na kuwapa Misri uongozi wa kundi G lenye timu zingine za Zimbabwe na Guinea zitakazocheza hapo kesho jijini Harare, Zimbabwe.
Misri mabingwa wa mara 7 barani Afrika wameshiriki fainali za kombe la dunia mara 2.
 
Nayo nchi ya Ghana chini ya kocha mzawa Kwesi Appiah ilipata ushindi mnono wa magoli 7-1 kwenye kundi D lenye miamba ya Afrika 2012, Zambia na Sudan, Ghana ilipata magoli yake kupitia kwa Sulley Muntari, Christian Atsu, Jeremiah Akaminko (1),huku  Dominic Adiyah na Jordan Ayew (2) kila mmoja.
 
Hii leo kutakuwa michezo kadhaa ikiwa na saa za hapa Tanzania kuanzia saa 10 kati ya Kenya dhidi ya Malawi hadi nne usiku Rwanda wakiikabili Algeria.


10:00 Kenya v Malawi Nairobi
11:00
Central African Republic
v Botswana Bangui
11:30 Cameroon v Congo DR Yaounde
01:30 Sierra Leone v Cape Verde Freetown
01:30 Gambia v Morocco Bakau
02:00 Sudan v Zambia Khartoum
02:00 Ivory Coast v Tanzania Abidjan
02:00 Tunisia v Equatorial Guinea Monastir
03:00 Burkina Faso v Congo Ouagadougou
03:00 Senegal v Liberia Dakar
04:30 Algeria v Rwanda Blida


No comments:

Post a Comment