KIKOSI cha timu ya
soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimewasili Abidjan huku Kocha Mkuu wa
timu hiyo Kim Poulsen akisema mechi dhidi ya Ivory Coast itakuwa ngumu.
Stars yenye wachezaji
21 ilikuwa iwasili hapa asubuhi, lakini ndege iliyobadilisha Nairobi ilichelewa
kuondoka kwa saa tatu. Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na
wenyeji Ivory Coast (Tembo wa Magharibi) itakayochezwa Juni 2 mwaka huu Uwanja
wa Felix Houphouet-Boigny kuanzia saa 11 kamili jioni ambapo Tanzania itakuwa
saa 2 kamili usiku.
Stars ililazimika
kuacha wachezaji wawili dakika za mwisho (Haruna Moshi na Nassoro Cholo), Kim
amesema kikosi chake ambacho kimefikia hoteli ya Ibis bado kimejipanga vizuri
kwa ajili ya mechi hiyo.
“Tunaiheshimu Ivory
Coast kwa vile ni timu ambayo inaundwa na baadhi ya wachezaji nyota wa dunia
kama akina Drogba (Didier) na Yaya (Toure), lakini wajiandaa kupata wakati
mgumu kutoka kwetu,” amesema Kim ambayo kikosi chake baada ya kuwasili hapa
kilipata fursa ya kufanya mazoezi jioni.
Kikosi cha Stars
kinaongozwa na Nahodha wake Juma Kaseja akisaidiwa na Aggrey Morris. Wachezaji
wengine waliopo hapa na kikosi hicho ni Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Amir
Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe na Juma
Nyoso.
Jonas Mkude, Mwinyi
Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher, Mrisho Ngasa,
Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva na John Bocco.
Mbali ya Kim, Benchi
la Ufundi lina Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa
makipa), Leopold Mukebezi (Meneja wa timu), Juma Mwankemwa (Daktari wa timu),
Frank Mhonda (Physiotherapist) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
Msafara wa Stars unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) Crescentius Magori lakini pia yupo Mwenyekiti wa Baraza la
Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi ambaye ameenda kushuhudia mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment