Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Mganda Hamis Kiiza anatarajiwa kurejea kwenye mngwe ya pili ya ligi kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kutimua vumbi kuanzia Januari 26 mwaka huu.
Nyota huyo wa mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati 2012, amesema kuwa, yuko fiti na anaendelea na mazoezi na timu yake ambayo siku ya Jumamosi itaikabili klabu ya Black Leopards ya Afrika Kusini katika mchezo wa majiribio kabla ya kuanza kwa ligi kuu Bara.
Klabu hiyi ilimaliza duru la kwanza ikiongoza kwenye msimamo mara baada ya kujikusanyia jumla ya alama 29 mbele ya Azam yenye alama 24 na Simba yeneye alama 23.
Kiiza maarufu kama Diego amefanikiwa kufunga jumla ya magoli manne kati ya 25 yaliyofungwa na klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam ambapo msimu uliopita alifunga jumla ya magoli mawili majira kama haya.
Nyota huyo pia amekanusha taarifa zinazomhusisha na kuihama klabu hiyo na kujiunga na mahasimu wao Simba SC mara baada ya dirisha la usajili kufunguliwa amesema anatarajia kufanya vizuri mzunguko huu wa pili kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo alifanikiwa kufunga mabao 12.

No comments:
Post a Comment