Guardiola, mwenye miaka 41, atachukua nafasi ya Heynckes, aliyekataa kuongeza mkataba na mimba hiyo ya Ujerumani na barani Ulaya mwezi Julai.
"Tumefurahi kufanikiwa kumshawishi mtu mwenye uwezo kama Pep Guardiola, ambaye amekuwa akitakiwa na vilabu mbalimbali vikubwa barani Ulaya, kujiunga na Bayern Munich," alisema mkurugenzi mkuu wa Bayern,Karl-Heinz Rummenigge hapo jana.
"Pep Guardiola ni miongoni mwa makocha wenye mafanikio ya juu kabisa duniani na natumaini ataleta tija kubwa kwa klabu yetu na soka la Ujerumani. aliongeza Rummenigge
Guardiola aliachana na miamba ya Uhispania kutoka jimbo la Katalunya, FC Barcelona msimu uliopita baada ya kuiongoza klabu hiyo kutwaa mataji 14 ndani ya misimu minne ikiwemo 2 klabu bingwa barani Ulaya, 3 ligi kuu nchini Uhispania na 1 klabu bingwa ya dunia.
Bayern kwa sasa inaongoza ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga ikiwa alama tisa mbele ya Bayer 04 Leverkusen ikiwa na alama 42 baada ya michezo 17 ya ligi hiyo.
Miongoni mwa matarajio ya wengi ni kuona TRINITY ya Barcelona baina ya Xavi, Iniesta na Messi ikihamia klabuni hapo huku Toni Kroos, Xherdan Shaqiri, na Bastian Schweinsteiger wakipewa nafasi kubwa ya kuwa chaguo la kocha huyo mpya.
Ligi hiyo intarajiwa kuendelea tena hapo kesho Ijumaa kwa Shalke 04 kuivaa Hannover 96, huku mechi zingine zikipigwa Jumamosi
| 19 Jan, 14:30 |
FSV Mainz 05
v
SC Freiburg
|
Coface Arena, Mainz | ||
| 19 Jan, 14:30 |
Bayern Munich
v
Greuther Fürth
|
Allianz-Arena, Munich | ||
| 19 Jan, 14:30 |
Bayer Leverkusen
v
Eintracht Frankfurt
|
BayArena, Leverkusen | ||
| 19 Jan, 14:30 |
VfL Wolfsburg
v
VfB Stuttgart
|
Volkswagen Arena, Wolfsburg | ||
| 19 Jan, 14:30 |
Hoffenheim
v
Borussia M’gladbach
|
Rhein-Neckar-Arena, Sinsheim | ||
| 19 Jan, 17:30 |
Werder Bremen
v
Borussia Dortmund
|
Weserstadion, Bremen | ||

No comments:
Post a Comment