VIEW OTHER SITES

Friday

20 ZAPATIKANA HATUA YA MTOANO ULAYA


 
Klabu kumi na nne zimefanikiwa kutinga hatua ya mtoano ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya kwa mwaka 2012/13 baada ya kumalizika kwa raundi ya tatu ya kufuzu kwa hatua hiyo ya mwisho ya mtoano inayojumuisha timu 20.
Miongoni mwa vilabu hivyo pia wapo mabingwa wa zamani wa ulaya Celtic FC, Fenerbahçe SK na FC Dynamo Kyiv.
Nayo, klabu ya RSC Anderlecht ya ubelgiji ilifuzu kwa kishindo baada ya kupata ushindi wa mabao 11-0 wa jumla dhidi ya FK Ekranas na kujikatia tiketi ya kushiriki hatua hiyo ya mtoano.
Timu nyingine ni FC Basel 1893 ya Uswizi, ambayo msimu uliopita walifika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo, huku FC BATE Borisov, GNK Dinamo Zagreb and CFR 1907 Cluj zikiikwaaa nafasi hiyo.
Mbali na klabu hizo zilizofuzu hatua hiyo kutokea raundi ya tatu, kati ya hizo zilizoingia hatua ya mtoano sita zinaingia nafasi hiyo moja kwa moja ambazo ni SC Braga ya Ureno, FC Spartak Moskva ya Urusi, Udinese Calcio ya Italia, Lille Metropole ya Ufaransa, Malaga CF ya Uhispania na Borrusia Monchengladbach ya Ujerumani.
Hatua hiyo ya mtoano inatarajiwa kuanza kati ya Agosti 21 na 22 huku mechi za marejeano zikichezwa kati ya Agosti 28 na 29.



UEFA Klabu bingwa hatua ya mtoano

SC Braga (POR)*
FC Dynamo Kyiv (UKR)
Panathinaikos FC (GRE)
FC København (DEN)
FC Spartak Moskva (RUS)*
Fenerbahçe SK (TUR)

Udinese Calcio (ITA)*
LOSC Lille Métropole (FRA)*
Málaga CF (ESP)*
VfL Borussia Mönchengladbach (GER)*
*zilizofuzu moja kwa moja hatua hiyo.
Mabingwa wa ligi zao.
FC Basel 1893 (SUI)
RSC Anderlecht (BEL)
Celtic FC (SCO)
FC BATE Borisov (BLR)
GNK Dinamo Zagreb (CRO)
CFR 1907 Cluj (ROU)
Helsingborgs IF (SWE)
NK Maribor (SVN)
AEL Limassol FC (CYP)
Hapoel Kiryat Shmona FC (ISRAEL)

No comments:

Post a Comment