Wachezaji
waliochaguliwa na jopo la makocha kwa kushirikiana na Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) na Chama cha Soka Dar es Saalam (DRFA), wakati wa
fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zilizofanyika kwenye Uwanja
wa Karume, Dar es Salaam Juni zilizoshirikisha timu kutoka mikoa ya
Lindi, Mbeya, Arusha, Ilala, Temeke na Kinondoni.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisi za TFF jana, Afisa Maendeleo wa Soka wa
TFF, Salum Madadi aliwataja vijana watakaowakilisha Tanzania kuwa ni
Denis Richard, Juma Hamza, Abdul Selemani, Ishaka Shekolowa na Bakari
Ally kutoka mkoa wa kisoka wa Temeke.
Wengine
ni Abdulatif Mohamed, George Joseph na Badilu Said (Lindi), Said
Kassim, Amos Ikungula, Paul Balama na Goodluck Mabiku (Ilala), Joel
Kasimula na Ibrahim Mtenga (Mbeya), Sntkony Angelo na Suleiman Yunus
(Arusha).
Mashindano
hayo yanayotarajiwa kuwa na ushindani mkali yatashirikisha wachezaji
wengine nyota wa ARS kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, DRC, Congo
Brazzaville, Nigeria, Ghana, Zambia, Niger, Gabon, Burkina Fasso,
Sierra Leone, Chad, Madagascar na Tanzania.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya, amesema
kuwa lengo la mashindano hayo ya kimataifa ni kuwapa vijana fursa
zaidi ya kuendeleza vipaji vyao na kupata uzoefu. “Vile vile Airtel
Rising Stars inatoa nafasi kwa wanasoka hawa chipukizi kuweza kupanua
jiografia yao na kujenga urafiki na vijana wenzao kutoka nchi
mbali
mbali”, alisema Singano.
Michuano
hiyo itafuatiwa na kliniki ya soka ya kimataifa ambayo itafanyika
Nairobi chini ya walimu wa soka la vijana kutoka klabu maarufu
duniani ya Manchester United ya Uingereza. Kliniki kama hii
ilifanyika mwaka jana kwenye uwanja wa kisasa wa soka jijini Dar es
Salaam na kushirikisha vijana kutoka Kenya, Malawi, Sierra Leone na
wenyeji Tanzania.
Katika
kliniki ya mwaka huu, Tanzania itawakilishwa na wachezaji sita
miongoni mwao ni wavulana watatu na wasichana watatu ambao walioibuka
kuwa wachezaji bora wakati wa fainali za Taifa jijini Dar es Salaam
mwezi Juni.
Airtel
Rising Stars ni mpango kabambe wa kuibua na kukuza vipaji vya
wanasoka wanaochipukia barani Afrika. Walengwa ni wavulana na
wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba ambao watapata fursa
ya pekee ya kuonyesha vipaji vyao mbele ya waatalum wa mpira wa miguu
wa kitaifa na kimataifa.
No comments:
Post a Comment