VIEW OTHER SITES

Friday

16 WATEULIWA AIRTEL RISING STARS YA TANZANIA

Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kupitia programu yake maalum ya kuvumbua na kukuza vipaji vya soka nchini ijulikanayo kama Airtel Rising Stars leo imetangaza kikosi cha wachezaji 16 watakaoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Airtel itakayofanyika jijini Nairobi kuanzia Agosti 19 hadi 25 mwaka huu.



Wachezaji waliochaguliwa na jopo la makocha kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Chama cha Soka Dar es Saalam (DRFA), wakati wa fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zilizofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam Juni zilizoshirikisha timu kutoka mikoa ya Lindi, Mbeya, Arusha, Ilala, Temeke na Kinondoni.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisi za TFF jana, Afisa Maendeleo wa Soka wa TFF, Salum Madadi aliwataja vijana watakaowakilisha Tanzania kuwa ni Denis Richard, Juma Hamza, Abdul Selemani, Ishaka Shekolowa na Bakari Ally kutoka mkoa wa kisoka wa Temeke.
Wengine ni Abdulatif Mohamed, George Joseph na Badilu Said (Lindi), Said Kassim, Amos Ikungula, Paul Balama na Goodluck Mabiku (Ilala), Joel Kasimula na Ibrahim Mtenga (Mbeya), Sntkony Angelo na Suleiman Yunus (Arusha).
Mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa na ushindani mkali yatashirikisha wachezaji wengine nyota wa ARS kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, DRC, Congo Brazzaville, Nigeria, Ghana, Zambia, Niger, Gabon, Burkina Fasso, Sierra Leone, Chad, Madagascar na Tanzania.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya, amesema kuwa lengo la mashindano hayo ya kimataifa ni kuwapa vijana fursa zaidi ya kuendeleza vipaji vyao na kupata uzoefu. “Vile vile Airtel Rising Stars inatoa nafasi kwa wanasoka hawa chipukizi kuweza kupanua jiografia yao na kujenga urafiki na vijana wenzao kutoka nchi
mbali mbali”, alisema Singano.
Michuano hiyo itafuatiwa na kliniki ya soka ya kimataifa ambayo itafanyika Nairobi chini ya walimu wa soka la vijana kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United ya Uingereza. Kliniki kama hii ilifanyika mwaka jana kwenye uwanja wa kisasa wa soka jijini Dar es Salaam na kushirikisha vijana kutoka Kenya, Malawi, Sierra Leone na wenyeji Tanzania.
Katika kliniki ya mwaka huu, Tanzania itawakilishwa na wachezaji sita miongoni mwao ni wavulana watatu na wasichana watatu ambao walioibuka kuwa wachezaji bora wakati wa fainali za Taifa jijini Dar es Salaam mwezi Juni.
Airtel Rising Stars ni mpango kabambe wa kuibua na kukuza vipaji vya wanasoka wanaochipukia barani Afrika. Walengwa ni wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba ambao watapata fursa ya pekee ya kuonyesha vipaji vyao mbele ya waatalum wa mpira wa miguu wa kitaifa na kimataifa.

OLIMPIKI ON TWITTER BOLT, RUDISHA NA REKODI ZA DUNIA


Congrats to the U.S. women’s soccer team for a third straight Olympic gold. So proud. –bo...


Congrats to the women of ! and : you’ve raised the bar again.
 
Pic: David Rudisha celebrates his unbelievable new 800m World Record. 1:40.91!


This gonna be a great season lakers miami chicago okc are ready for war



It's Day 14! The USA have won 16 of 22 gold medals in the men's 4x400m Relay, can they keep the trend going?


D.A. reports from London on Kobe finding his game, LeBron's presence, the quest for gold and more. Video:


Usain Bolt: fastest man to ever live?


GMs around NBA questioning 2 things: 1. Orlando's motivation. 2. Whether Dwight re-signs with 35-year-old Kobe & 39 y/o Nash next yr


Here's everything you need to know about the reported -to-Lakers deal ->

Kuelekea mchezo wa fainali kati ya Marekani dhdi ya Argentina hii leo

: ready for Argentina, Friday at 4pm/et. VIDEO:


Tottenham Hotspur's preparations for the new Premier League season continued with a 2-0 defeat away to Valencia.

gold: Spotakova (CZE) wins women’s Javelin Throw. Germany’s Obergfoll & Stahl take silver and bronze

More gold!: A convincing women’s 72kg win for Vorobieva (RUS) who defeats Hristova (BUL) 5-0

Thank you bolt.. Thank you 

Congratulations Usain, you deserve it bro.


Well done kenya for WR 

MNAZI WA GUNNERS KUFUATIA UJIO WA CAZORLA EMIRATES
Santi Cazorla, Alex Song, Mikel Arteta, Jack Willshere, Thomas Rosicky, Aaron Ramsey, Abou Diaby Best Midfield in EPL?? Without a doubt!

 
 
 

MISIMAMO MAKUNDI KUELEKEA BRAZIL 2014 BAADA YA RAUNDI YA PILI


Kundi A
TimuMPWDLGFGAPts
Ethiopia2110314
Central African Republic2101223
South Africa2020222
Botswana2011131

Kundi B
TimuMPWDLGFGAPts
Tunisia2200526
Sierra Leone2110434
Equatorial Guinea2011351
Cape Verde Islands2002240

Kundi C
TimuMPWDLGFGAPts
Côte d'Ivoire2110424
Tanzania2101233
Morocco2020332
Gambia2011231

Kundi D
TimuMPWDLGFGAPts
Sudan2110204
Ghana2101713
Zambia2101123
Lesotho2011071

Kundi E
TimuMPWDLGFGAPts
Congo2110104
Gabon2110104
Burkina Faso2011011
Niger2011011

Kundi F
   TimuMPGroupWDLGFGAPts
Nigeria2110214
Namibia2101113
Malawi2020112
Kenya2011011

Kundi G
TimuMPWDLGFGAPts
Egypt2200526
Guinea2101333
Zimbabwe2011011
Mozambique2011021

Kundi H
TimuMPWDLGFGAPts
Benin2110214
Algeria2101523
Mali2101223
Rwanda2011151

Kundi I
TimuMPWDLGFGAPts
Libya2110324
Congo DR2101213
Cameroon2101223
Togo2011131

Kundi J
TimuMPWDLGFGAPts
Senegal2110424
Uganda2020222
Angola2020112
Liberia2011131

20 ZAPATIKANA HATUA YA MTOANO ULAYA


 
Klabu kumi na nne zimefanikiwa kutinga hatua ya mtoano ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya kwa mwaka 2012/13 baada ya kumalizika kwa raundi ya tatu ya kufuzu kwa hatua hiyo ya mwisho ya mtoano inayojumuisha timu 20.
Miongoni mwa vilabu hivyo pia wapo mabingwa wa zamani wa ulaya Celtic FC, Fenerbahçe SK na FC Dynamo Kyiv.
Nayo, klabu ya RSC Anderlecht ya ubelgiji ilifuzu kwa kishindo baada ya kupata ushindi wa mabao 11-0 wa jumla dhidi ya FK Ekranas na kujikatia tiketi ya kushiriki hatua hiyo ya mtoano.
Timu nyingine ni FC Basel 1893 ya Uswizi, ambayo msimu uliopita walifika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo, huku FC BATE Borisov, GNK Dinamo Zagreb and CFR 1907 Cluj zikiikwaaa nafasi hiyo.
Mbali na klabu hizo zilizofuzu hatua hiyo kutokea raundi ya tatu, kati ya hizo zilizoingia hatua ya mtoano sita zinaingia nafasi hiyo moja kwa moja ambazo ni SC Braga ya Ureno, FC Spartak Moskva ya Urusi, Udinese Calcio ya Italia, Lille Metropole ya Ufaransa, Malaga CF ya Uhispania na Borrusia Monchengladbach ya Ujerumani.
Hatua hiyo ya mtoano inatarajiwa kuanza kati ya Agosti 21 na 22 huku mechi za marejeano zikichezwa kati ya Agosti 28 na 29.



UEFA Klabu bingwa hatua ya mtoano

SC Braga (POR)*
FC Dynamo Kyiv (UKR)
Panathinaikos FC (GRE)
FC København (DEN)
FC Spartak Moskva (RUS)*
Fenerbahçe SK (TUR)

Udinese Calcio (ITA)*
LOSC Lille Métropole (FRA)*
Málaga CF (ESP)*
VfL Borussia Mönchengladbach (GER)*
*zilizofuzu moja kwa moja hatua hiyo.
Mabingwa wa ligi zao.
FC Basel 1893 (SUI)
RSC Anderlecht (BEL)
Celtic FC (SCO)
FC BATE Borisov (BLR)
GNK Dinamo Zagreb (CRO)
CFR 1907 Cluj (ROU)
Helsingborgs IF (SWE)
NK Maribor (SVN)
AEL Limassol FC (CYP)
Hapoel Kiryat Shmona FC (ISRAEL)