VIEW OTHER SITES

Thursday

STARS YAWASILI MSUMBIJI KUIKABILI MAMBAS


Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” kimewasili nchini Msumbiji bila nyota wake watatu wenye majeraha kwenye mchezo wa marejeano utakaopigwa Jumapili hii.
Msemaji wa shirikisho la soka nchini (TFF), Boniface Wambura amesema kuwa nyota watakaokosa mchezo huo ni pamoja na mlinda lango namba mbili, Mwadini Ali, mlinzi Nassoro Said “Chollo” na Waziri Salum ambao wote wana majeraha huku Chollo akitarajiwa kuwa nje kwa takribani msimu mzima.
Mchezo huo utapigwa majira ya saa 10 jioni sawa na saa 11 jioni za hapa nchini kwenye uwanja wa Zimpeto uliopo jijini Maputo nchini humo.
Awali timu hizo zilitoka suluhu ya 1-1 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Februari, 29, akielezea kuelekea mchezo huo kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema, “ Tunahitaji mmalizaji dhidi ya Msumbiji na natumaini washambuliaji watafanya kazi nzuri wakati huu tikutaka kupata matokeo mazuri.”
Kikosi hicho kitashuhudia urejeo wa beki wake, Aggrey Morris ambaye alikosekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Gambia kutokana na kusimamishwa kwenye mchezo dhidi ya Ivory Coast.
Wengine watakaopatikana ni pamoja na kiungo Nurdin Bakari na mshambuliaji Thomas Ulimwengu ambao hawakucheza mechi zilizopita kutokana na majeraha waliyoyapata.




No comments:

Post a Comment