Klabu ya Simba huenda
ikawaacha nyota wake akiwemo beki wa kulia, Nassor Masoud ‘Chollo’ na kipa
William Mweta kutokana na ripoti ya daktari wa klabu hiyo, Cossmas Kapinga kuonesha
kuwa nyota hao wawili ni wajeruhi wa muda mrefu.
“Ripoti
niliyoiwasilisha kwa uongozi nimesema wazi kuhusu wachezaji hao, kwamba ni
majeruhi wa muda mrefu, wanaweza kuwa nje miezi zaidi ya mitatu,”alisema
Kapinga hii leo.
Taarifa za ndani za
klabu hiyo zinaonesha kuwa nyota hao huenda wakatemwa baada ya kupatikana kwa
wachezaji wenye uwezo wa kuziba nafasi zao akiwemo Shomari Kapombe ambaye
anauwezo wa kucheza kama beki wa pembeni.
“Hawataachwa moja kwa
moja, wataendelea kuhudumiwa na klabu, kila kitu kulingana na mikataba yao, ila
wataondolewa kwenye usajili, kwa sababu watakuwa wanajaza nafasi wakati
hawawezi kucheza.
Klabu itawahudumia
vizuri, wakipona kama mzunguko wa pili au hata msimu ujao, watarudishwa kikosini,”alisema
mmoja wa wajumbe wa klabu hiyo.

No comments:
Post a Comment