VIEW OTHER SITES

Tuesday

UHAI KURINDIMA DESEMBA 7


Mashindano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi  kuanziaDesemba 7, mwaka huu kwenye viwanja vya Karume,jijini Dar es Salaam.

Mashindano haya hudhaminiwa na kampuni ya Azam, ambao ni watengenezaji na wasambazaji wa maji ya Uhai, yanatarajiwa kufikia tamati Desemba 22 mwaka huu.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura amesema kuwa, wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ni wale ambao usajili wao umefanyika TFF na kupatiwa leseni.
“Hakutakuwa na usajili mwingine wowote mbali na ule uliofanyika sambamba na wa Ligi Kuu. Taratibu zote za michuano hiyo zitafahamishwa kwa klabu husika ikiwemo ratiba ya michuano hiyo,”alisema

Mashindano hayo msimu uliopita yalishudia timu ya vijana ya Simba ikitwaa ubingwa kwa kuishinda Azam U20 kwa jumla ya penati 6 - 5.

No comments:

Post a Comment