Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba SC, Mghana Daniel Akuffor amethibitishwa kuwa yuko vizuri kwa mchezo dhidi ya Azam katika Ngao ya Jamii utakaopigwa kesho
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akuffor aliumia Alhamisi
iliyopita baada ya kugongana na mchezaji wa Sofapaka ya Kenya katika eneo
la moyo na kusababisha ulimi wa mchezaji huyo kugeuka na kuziba njia ya
kupitisha hewa.
Akizungumza na blog hii daktari wa Simba, Cosmas Kapinga,
amesema mchezaji wao yuko katika hali ya kawaida ambapo jana aliweza kufanya
mazoezi na wenzake.
Kapinga ameongeza kuwa mara baada ya kuzimia uwanjani mchezaji
huyo alifanyiwa uchunguzi na hakukuwa na tatizo alilokutwa nalo kutokana na tukio lililotokea uwanjani ni sehemu ya matukio yanayotokea sehemu
mbalimbali.
"Hana tatizo lolote, yuko fiti kucheza Jumanne (kesho) na hata kama leo
(jana) kungekuwa na mechi angeweza kupangwa," alisema Kapinga.
Pia ameeleza kuwa mchezaji huyo hana historia na kusumbuliwa na moyo na
kilichotokea ni hali ya kawaida ambayo ingeweza kumtokea mchezaji
yoyote.
Upande wake Akuffour alisema, "Naweza kucheza, namshukuru Mungu nimepona,"
Simba na Azam zitakutana kesho majira ya saa 10:00 jioni katika mchezo wa ufunguzi
wa Ligi ya Bara maarufu kama Ngao ya Jamii huku ligi ikianza rasmi Jumamosi kwa timu zote 14 kushuka
viwanjani.
No comments:
Post a Comment