Timu ya Pemba Kaskazini imepokea kichapo cha magoli matatu bila majibu mbele ya vijana wa Mkwawa, Iringa kwenye mchezo wa mashindano ya Copa Coca-cola kwa vijana chini ya miaka 17 hii leo kwenye uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani.
Magoli ya Iringa yamewekwa kimiani na Goodluck Jonas dakika ya 51, Musa Maginga dakika 67 na Ramadhan Kiwelu dakika ya 70.
Mechi mbili zilizopita Iringa ilipata kichapo cha 3-1 kutoka kwa Mwanza na 3 -0 kutoka kwa Mjini Magharibi, huku, Tabora ilishinda kwa goli mbili bila majibu dhidi ya Shinyanga kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kupitia kwa Said Juma na ramadhani Mbalamwezi.
Nayo Ilala imeona mwezi hii leo baada ya kutoka suluhu tasa dhidi ya Kusini Pemba kwenye uwanja wa Tanganyika Packers mchezo wa kundi A uliopigwa jijini Dar es Salaam wakati, mjini Kibaha mkoani Pwani kwenye uwanja wa TAMCO, Dodoma ilishinda 1-0 dhidi ya Mtwara.

No comments:
Post a Comment