Klabu ya Simba imepata
pigo baada ya kuumia kwa beki wake wa kulia,Nassor Masoud ‘Chollo’ ambaye atakuwa nje kwa
wiki sita.
Daktari wa Simba SC,
Cossmas Kapinga amesema kuwa beki huyo alifanyiwa vipimo na kubainika kuwa
atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki sita, jambo litakalomfanya kukosekana hadi
michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Chollo ameumia mfupa
wa katikati ya goti, hali iliyowakuta beki wa zamani wa Simba, Mganda Joseph
Owino ambaye amehamia Azam FC na kiungo aliyeongeza mkataba hivi karibuni,
Uhuru Suleiman ambao walilazimika kuwa nje ya Uwanja kwa msimu mzima.
“Tofauti yake Chollo
na akina Owino ni kidogo sana, yeye (Chollo) haujavunjika wote, lakini wenzake
ulivunjika wote, pamoja na yote wiki sita ni nyingi. Anaweza asionekane kanisa
uwanjani mwaka huu, kwa sababu hadi apone aanze taratibu, ni mtihani,”alisema
Kapinga akizungumzia hali zilizowakuta wachezaji hao.

No comments:
Post a Comment